Wamachinga hawasaidii Tanzania!

Wamachinga hawasaidii Tanzania!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!

1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.

2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.

3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.

4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.

5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
 
Wee mtu ni mjinga sana wakati mwingine. Vijana wanajituma kwa kujiajiri wenyewe. Huoni hilo ni bora kuliko kukaa kijiweni kuvuta bangi na kupiga raia vitofali usiku? Hata boda nao utasema hawana faida.

Umekaa Texas miaka na miaka unafanya kazi kama nesi sjui yena Mwanaume mzima na ni wazi umepoteza ukaribu na uhalisia wa maisha Tanzania.
 
Vijana wameamua kujishughulisha wasikae bure, kipato wanachopata ni msaada tosha kwa taifa
 
Hata hao unaowaona wafanyabishara wakubwa wengi wameanzia kwenye umachinga.. hiyo ni njia tu ya kufikia malengo.

Halafu kumbuka kila huduma anayonunua analipa kodi, hata hizo bidhaa unazoziita za kijinga zimelipiwa kodi pale bandarini.

Akinunua sigara, mafuta, sukari,sabuni na vinginevyo vinakodi ndani yake..
 
Wee mtu ni mjinga sana wakati mwingine. Vijana wanajituma kwa kujiajiri wenyewe. Huoni hilo ni bora kuliko kukaa kijiweni kuvuta bangi na kupiga raia vitofali usiku? Hata boda nao utasema hawana faida. Umekaa Texas miaka na miaka unafanya kazi kama nesi sjui yena Mwanaume mzima na ni wazi umepoteza ukaribu na uhalisia wa maisha Tanzania.
Huyo jamaa huwa ana mada zake za ajabu ajabu sana.

Sijui kama huwa anamkakati wowote na hizi mada au la, lakini kuna aina fulani ya mfanano ukizifuatilia vizuri.

Kuna wakati aliandika kulaumu vijana wa kiTanzania wasivyojituma na kuchangamkia fursa, akilinganisha na vijana wa nchi aliyozaliwa yeye. Leo analalamika kwa hawa vijana kujishughulisha na kilichopo wanachoweza kukifanya.

Sasa sijui kama ni kwa bahati mbaya, au ndivyo zilivyopangiliwa.
 
SAWA.
Lakini ni nani hasa alaumiwe, machinga, au hao wasioweza kufanya mipango ya kuigeuza hali ya umachinga na kuwa fursa ya kuwajengea uwezo wahusika?
 
Yaani haya mambo ni fikirishi....naona tumebakia taifa la wachuuzi tu, wengi wao wakiwa vijana wenye nguvu ambazo zingeweza kutumika kufanya uzalishaji wenye tija kupitia kilimo ,viwanda nk. ili kujenga uchumi endelevu na wa uhakika.......
 
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!...
Wacha watu wajiajiri ili maisha yasonge. Usiwaze kodi tu
 
Wee mtu ni mjinga sana wakati mwingine. Vijana wanajituma kwa kujiajiri wenyewe. Huoni hilo ni bora kuliko kukaa kijiweni kuvuta bangi na kupiga raia vitofali usiku? Hata boda nao utasema hawana faida.

Umekaa Texas miaka na miaka unafanya kazi kama nesi sjui yena Mwanaume mzima na ni wazi umepoteza ukaribu na uhalisia wa maisha Tanzania.

Naona badala ya kujadili hoja unajaribu kinijadili mimi.

1. kwanza hujabisha chochote. Wamachinga ni bora wangekaa vijiweni biashara za walipa kodi zingebaki na kodi kuongezeka, uchafu ungepungua na gharama za kusafisha ambazo sasa hawakipi na wamekuwa kama wauzaji wa vitu vya china ambavyo havina viwango! Kama unahoja jadili
2. Kuhusu mimi: Kwanza ni kweli nipo Texas tena nikusaidie nipo Dallas, Texas. Pili mimi sijawahi kuwa nurse wala kusoma masomo ya sayansi! Sijui umetoa wapi mambo ya mimi kuwa Nurse. Nilishawahi kuandika hapa mawazo yangu kwa wizara ya afya Tanzania na nikisema kwamba mimi nimesoma Finance na ni na nashughulikia mambo ya supply chain sasa sijui kuwa Nurse imetoka wapi. Usipoteze muda mwingi kwenye umbea tusaidie nchi yetu
3. Vijana wengi ni wa vivu. Ni lini vijana wamekutana kama kikundi na kuomba mashamba ya ujasiliamali kwa serikali wakanyimwa. Lakini kitu kingine vijana sio waaminifu wanafikiria kuiba sana na hili linawarudisha nyuma kwenye kazi za kufanya pamoja.

Huu ndiyo ukweli ni ulalamishi tu kila siku kwa watu wengine
 
You can say that again and again Mkuu.

Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!

1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.

2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.

3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.

4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.

5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
 
..mwaka 2015 nilipomsikia mgombea uraisi wa ccm anasema anataka kujenga Tanzania ya viwanda nilitarajia kwamba ktk uongozi wake wamachinga wengi watapata ajira rasmi viwandani na idadi yao itapungua mwaka hadi mwaka.
 
Huo ndio ukweli mchungu. Wamachinga wanaelemea taifa na kuchukua haki za walipa kodi wengine. Ni muda sasa kama Taifa kuwatafutia shughuli nyingine ya uzalishaji itakayo walipa na kuwaondoa barabarani.
 
Back
Top Bottom