Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Viongozi wa juu wamewapa vichwa wamachinga sasa wamachinga hawamsikilizi mtu yeyote pamoja na wao.Wapewe maeneo rasmi ya biashara wasiachwe kusambaa kila mahali..NI KERO
Hawakujiita wao bali mwendazake ndiye aliyewabatiza hivyo nao wakafurahia jina hilo ambalo sasa linaigharimu serikali.Na hii tabia ya kujiita wanyonge imeshakuwa sugu. Unyonge siyo ID
Hili tatizo lililelewa na kayafaViongozi wa juu wamewapa vichwa wamachinga sasa wamachinga hawamsikilizi mtu yeyote pamoja na wao.
Mzaha mzaha litakuja kuleta mapigano makubwa kati yao na polisi, tukumbuke kunasiku walimuua mfanyabiashara wa Kariakoo baada ya gari yake kukanyaga nyanya kwa bahati mbaya na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa.Hili tatizo lililelewa na kayafa
Hili tatizo lililelewa na kayafa
Inatia hasira halafu inaudhi mnoBarabara ya Zakhiem Mbagala Rangitatu ina vibanda vingi vya wamachinga kando ya kuta za viwanda, wamachinga hawa wanalindwa na mamlaka kwa hali na mali kwa sababu ndio wapiga kura wetu.
Wapigakura hawa wenye vibanda nyakati za usiku hugeuka nguchiro na kuanza kutoboa kuta za viwanda kwa ajili ya kuiba ndani ya viwanda, huu ndio uwekezaji mkubwa wa wapigakura wetu hawa na kiwanda kilichoathirika sana ni cha Maji Poa.
Tatizo hili si huko tu hata maduka yanayobanwa na wamachinga nayo hukabiliwa na wizi wanaotumia mbanano kuwa kinga.
Hap TARURA ndio hovyo kabisaa kazi yao kuvizia magari yanayoegesha pembezoni mwa barabaraNa Hawa viongozi tuliobaki nao wote wamelemaa na ugonjwa huu wa kuwaacha wamachinga wavunje taratibu zetu bila kuchukuliwa hatua, karibu miji yote na halmashauri nyingi tu zimevamiwa na wahusika Tarula, tanroad, halmashauri, Police, maDiwani , mgambo, ...etc hakuna anayewajibika, angalia leo inchi nzima tatizo la bodaboda Linavyosumbua traffic ambao Sasa Ni wazi kuwa hawana control nao
TARURA hawawezi kuwagusa wamachinga na hakuna anayeweza kuwagusa isipokuwa Rais tu, hata Waziri Mkuu hana ubavu wa kuwagusa wamachinga. Tunamsikia Mkuu wa Mkoa akijibaraguza kuhusu wamachinga lakini huishia kuwatuma Wakuu wa Wilaya huku akijua hawawezi kuwafanya kitu, serikali imewajengea jeuri ambayo inahatarisha usalama wa wananchi wengine. Jana nilimsikia Mkuu wa Mkoa Dar. akifikiria uwezekano wa kufunga baadhi ya mitaa ili itumiwe na wamachinga! Nilijiuliza kuhusu wakazi wa mitaa hiyo pamoja na wenye maduka, je, watahamishwa? Ni wazi kauli ile ni ya kutapatapa.Hap TARURA ndio hovyo kabisaa kazi yao kuvizia magari yanayoegesha pembezoni mwa barabara
Duh!Mzaha mzaha litakuja kuleta mapigano makubwa kati yao na polisi, tukumbuke kunasiku walimuua mfanyabiashara wa Kariakoo baada ya gari yake kukanyaga nyanya kwa bahati mbaya na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa.