Wamachinga waomba kukutana na Rais Samia

Tatizo hili la watu kufanya biashara katika sehemu zisizo rasmi ni lazima lichukuliwe kwa uzito wake kwamba kufanya hivyo ni kuvunja sheria na katu lisivhukuliwe kisiasa. Hawa wamachinga wengi wao kwa kufanya biashara zao wanachafua miji na makazi ya watu na pia huzikosesha halmashauri mapato mengi.
Hili la kuzikosesha halmashauri mapato nitalizungumzia kwa mifano halisi kutoka wilaya ya Kinondoni. Katika wilaya ya Kinondoni kwenye ramani za sehemu mbali mbali mfano Mbezi Beach kuna maeneo yaliyotengwa kutumika kama masoko lakini kuna wenye viwanja vya makazi wamevigeuza kuwa sehemu za wamachinga kufanya biashara zao na wao kukusanya mapato ambayo yaliyakiwa yaende kwenye halmashauri lakini yanaingia mifukoni mwa watu . Ukienda pale Mbezi Beach sehemu ijulikanayo kwa jina la Rungwe utakuta vibanda vingi na karakana pia vitu ambacho sio rasmi kuwepo hapo.

Uongozi wa Kinondoni ichukue fursa hii kusafisha wilaya yake kwa kuhakikisha kuwa viwanja vya makazi vinatumika hivyo na sio vinginevyo na pale sheria inapovunjwa pasiwe na double standard hata kama muhusika ni mke wa Rais!
 
Machinga kumbe walikuwa wanachafua barabara za miji sana sanaaa, yaani sasa hivi ukipita barabara za mitaa ya Posta, kote Kkoo, Tandika, kote, barabara zinapitika, safiii, msongamano hakuna, yaani kama ulaya au Marekani vile, nimeamini kumbe ukiwapanga hawa machinga hata sura ya barabara na miji inaonekana na usafi na hata usalama unaonekana mtu si rahisi kukuibia iwe mchana au usiku.

Machinga wasikilize serikali wapangwe maeneo yao maalum na ya sokoni. Sio kukaa mabarabarani, kila kona yaani walikuwa wameziba kila kona, barabara kama soko. Sasa at least Mh. Rais wetu Mama Samia kwa hili tunakupongeza sana sanaa.
 


Kuna mapato mengi sana yatokanayo na faini ambayo mamlaka yangezipata kwa wale wanaovunja sheria. Wengine wanaweka mabango, wengine wanapaki magari, wengine wanafanya biashara hadi zingine hatarishi kama kuwasha moto, kupika vyakula hadi wengine wanachoma vyuma.

Wote hawa ni kuwapiga faini kali tu. Hauhitaji kukimbizana nao.

Unawapa upendeleo watu ambao kwanza inawezekana kipato chao wengine ni kikubwa sana ila kwa kuwa wamejipachika label ya Machinga wanaonekana 'wanyonge'.

Kuna watu wana fremu au wanajaribu kupata vipato kwa njia halali ila wana vipato vya chini kuliko hawa wanaitwa 'Machinga'.
 
Mkuu hizi ndo mbinu za serikali. KUTENGENEZA TATIZO > KUSOLVE TATIZO > KUJINYAKULIA UMAARUFU.
 
Ili wazibe mitalo nakupanga vitu vikizuia kuona maduka ya wengine?
 
Marehemu alikuwa mtu wa hovyo hovyo sana, katuachia msala!!
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Sasa hili ni jipu.
 
inamaana MKuu wa Mkoa ndg. Makala kashindwa kazi?!
Kabla ya kukutana na Rais kuna viongozi wengi tu wa kuwasikiliza,
1. Kuna Mkuu wa Mkoa, Mbunge, Madiwani.
2. Waziri wa Viwanda na Biashara, Naibu, katibu mkuu.
3. Waziri Mkuu
4. Makamu wa Rais.

Tusijenge mazoea ya kuruka ngazi, tujifunze utaratibu wa kuheshimu ngazi/utaratibu.
 
Ukiachana na yote hili suala la wamachinga ni la kimaslahi zaidi hapo kariakoo watu wa maduka wanalipa Kodi za kutosha serikalini na bado biashara zao haziend maana sehem kubwa ya wateja hupenda kununua Kwa hawa watu ambao bei zao ni pozo sana kwakua wengine hata Kodi hawalipi lamda ushuru Tu Kwa baadhi Yao.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…