SoC02 Wamachinga wenzangu tubalidilike, tuachane na mtazamo wa kuona kama tunaonewa

SoC02 Wamachinga wenzangu tubalidilike, tuachane na mtazamo wa kuona kama tunaonewa

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 2, 2022
Posts
60
Reaction score
75
UTANGULIZI
Wamachinga tuna umuhimu sana katika kukuza pato la Taifa na takwimu zinaonesha kuwa sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo imetengeneza ajira, kukuza uchumi na kuondoa umasikini. Chapisho hili nimeliandika kwa lengo la kuwataka wamachinga wenzangu tubadilishe mitazamo ya kuona kama tunaonewa tunapotolewa katika mazingira ambayo sio rasmi kwa biashara zetu ndogondogo na kupelekwa katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya kufanya biashara kwani mara nyingi tumekuwa tukifanya biashara zetu kwenye mazingira ambayo sio rasmi na muda mwingine ni hatarishi kwa usalama wetu na usalama wa watu wengine.

Hivyo basi katika andiko hili nitaelezea maeneo yaliyopigwa marufuku kwa biashara zetu kama wamachinga na athari zake pamoja na maeneo tuliyotengwa kufanya biashara na faida za kufanyia biashara katika maeneo yaliyotengwa na serikali.

MAENEO YALIYOPIGWA MARUFUKU WAMACHINGA KUFANYIA BIASHARA
(a) Wamachinga tumepigwa marufuku kufanya biashara katika hifadhi ya barabara ambapo wamachinga wengi tumekuwa tukipanga na kuuza bidhaa pembezoni mwa hifadhi ya barabara wanakopita waenda kwa miguu na muda mwingine tunafanya biashara hata katikati ya barabara.

(b) Wamachinga tumepigwa marufuku kufanya biashara nje ya maduka, kwenye kuta za Hospitali, vituo vya Afya na mashule yanatakiwa kuwa wazi, ili kuruhusu shughuli za maeneo hayo zifanyike kwa umakini zaidi.

(c) Vilevile wamachinga hatupaswi kufanya biashara katika maeneo mengine yoyote ambayo ni hatarishi kwa usalama wetu na watu wengine kama pembezoni mwa reli, chini ya nguzo za umeme pamoja na maeneo mengine hatarishi.

ATHARI ZA KUFANYA BIASHARA KATIKA MAENEO YALIYOPIGWA MARUFUKU
Uwepo wa Machinga katika maeneo yasiyo umekuwa na athari nyingi ambazo ni:

(a) Husababisha kusimama kwa shughuli zingine hususani pale wamachinga tunapofanya biashara zetu nje ya maduka, kwenye kuta za Hospitali, na mashule au mbele ya Ofisi za Taasisi zingine za serikali au zisizo za serikali tunasabaisha shughuli hizo zisifanyike kwa umakini kwa sababu tunawazuia wateja wanaoingia na kutoka.

(b) Kongezeka kwa ajali hususani ajali za barabarani ambapo wamachinga tunapofanya biashara pembezoni mwa barabara husababisha baadhi ya wapita njia kugongwa na magari kutokana na kulazimika kupita barabarani na muda mwingine sisi wenyewe wamachinga tunaweza kugongwa na magari. Ajali zingine zinaweza kutokea ni ajali za umeme kwa wamachinga wanaofanyia barabarani chini ya nguzo za umeme na ajali ya Treni kwa wanaofanyia biashara pembezoni mwa reli.

(c) Kuongezeka kwa misongamano isiyokuwa na tija jambo ambalo linaweza kusababisha kusambaa kwa baadhi ya magonjwa kama Ugonjwa wa Uviko 19 ambao husambaa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

(d) Uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya kutupa taka ovyo katika mitalo ya barabara na maeneo yasiyo rasmi kutokana na uwepo wa baadhi ya Machinga na wateja wetu hutupa taka kinyume na utaratibu jambo ambalo linaweza kusababisha kuzuka kwa magojwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA WAMACHINGA
Maeneo ya kufanyia bishara kwa wamachinga ni yale yaliyotengwa na Halmashauri ili kuwawezesha Wamachinga kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi. Ambapo masoko mazuri na ya kisasa yenye miundombinu iliyoimara kama vile miundombinu ya vyoo, uwekwaji wa taa, na kujenga miundombinu ya kuweka taka katika maeneo hayo.

Masoko hayo yametengwa kwa ajili ya wamachinga kufanya biashara na kuhakikisha mazingira bora kwa wamachinga kufanya biashara zao katika maeneo stahiki. Vilevile wamachinga tumekuwa tukipewa kipaumbele cha kupewa nafasi ya kufanyia biashara katika masoko yaliyotengwa kwa ajili ya biashara ndogondogo.

FAIDA ZA WAMACHINGA KUFANYA BIASHARA KATIKA MAENEO YALIYOTENGWA NA SERIKALI
Wamachinga tunapofanya biashara zetu katika maeneo yaliyopangwa na serikali tunapata faida mbali ambazo ni:

(a) Kupungua kwa ajali mbalimbali hususani ajali za barabarani kwani watembea kwa miguu hawatokuwa wanatembea tena barabarani badala yake watatembea katika njia zao. Vilevile wamachinga wataondokana na kugongwa na magari kwani hawatokuwa wanafanya biashara katika hifadhi za barabara.

(b) Kuendelea kwa shughuli zingine za kimaendeleo kwa sababu wamachinga hatutokuwa tunafanya biashara mbele ya maduka, kwenye kuta za Hospitali, na mashule au mbele ya Ofisi za Taasisi zingine za serikali au zisizo za serikali hivyo wateja wanaweza kuingia na kutoka bila ghasia yoyote.

(c) Misongamano isiyokuwa na inaweza kupungua kwa sababu wamachinga tutakuwa katika maeneo maalum yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya kufanyia biashara zetu jambo ambalo linaweza kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa Uviko 19 ambao husambaa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

(d) Kutasaidia utunzaji wa mazingira kwa sababu ya kuwepo kwa miundombinu iliyoimara kama vile miundombinu ya vyoo, na miundombinu ya kuhifadhi taka jambo ambalo linaweza kusaidia kupungua kwa magojwa ya mlipuko kama vile kipindupindu ambayo husabishwa na uchafuzi wa mazingira.

HITIMISHO
Kwa kumalizia niwaombe wamachinga wenzangu tuachane na kasumba ya kuona kama tunaonewa tunapotolewa katika mazingira ambayo sio rasmi kwa biashara zetu na kupelekwa katika maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya kufanya biashara kwa usalama wetu kwani tunapofanya biashara katika maeneo yasiorasmi tunahatarisha usalama wetu na wa watu wengine pamoja na kukwamisha shughuli zingine za kimaendeleo.

Vilevile Serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali wa biashara iwape elimu wamachinga pamoja na kuongeza idadi ya masoko kwa ajili ya wamachinga kwani Idadi ya masoko kwa ajili ya wamachinga yaliopo sasa hivi ni machache kulinganisha na idadi ya wamachinga waliopo nchini.
 
Upvote 4
Kiukwel machinga wanaonewa sio kama.awamj ilopita.
Naomba unipgie kura pia
sawa kaka
 
Ukishiba unakuja kuandika hapa utumbo kwahiyo sikuungi mkono
Mwanasayansi kwahiyo ujataka wamachinga tuendelee kukaa barabarani na kusababisha misongamano isiyokuwa na tija na muda mwingine tusababishe hata ajali badilisha fikra.
 
Mwanasayansi kwahiyo ujataka wamachinga tuendelee kukaa barabarani na kusababisha misongamano isiyokuwa na tija na muda mwingine tusababishe hata ajali badilisha fikra.
Kwa uchumi tulio kuwa nao nisawa sasa aondoke akauze wapi lazima aangalie sehemu ya kuuzia hata hii hali ilishawai kuwepo marekani mnamo mwaka 1940. Hatuwezi kujifafananisha na marekani wakati wao kwenye uchumi wameanza mda kuliko sisi.

Na unakuta sehemu walizo pangiwa wamachinga ni sehemu ambazo hazina wateja kwa siku mmachinga anaingiza shilingi miambili tu unazani atakuja kula wapi kwa miambili ?
 
Vipi kuhusiana na maeneo mliyotengewa wateja wapo au ndo wa kuhesabu?
Wateja wapo kwa kutumia kiasi chake na hiyo ni kwa sababu kuna baadhi ya wamachinga bado wapo wanaofanyia biashara katika maeno yasiyo rasmi ndio wanawazuia wateja kuja sokoni. iwapo wamachinga wote tutafanyia biashara katika maeneo yaliyotengwa ninaimani wateja watakuwa wengi zaidi maana bidhaa zote zitakuwa zinapopatikana kwenye masoko yaliyotengwa.
 
  • Thanks
Reactions: Edw
Back
Top Bottom