Nawahusisha wamakonde wote wote katika mada hii na dharau anayoipata HALILA TONGOLANGA--FIELD MARSHAL TONGOLANGA (R.I.P)
1. Aliwatambulisha sana wamakonde Tanzania hii kupitia sanaa yake. 'kila munu ave na kwao' miaka ile ilifanya wamakonde mfuatwe majumbani kule dar na watu mbalimbali wa makabila mengine wakitaka kutafsiriwa maneno yaliyotumika mle.......kimakonde haikuwa lugha ya ajabu tena masikioni mwa watu.
2. Ngoma yenu ya asili, 'sindimba', nayo ikazidi kupaa kupitia yeye!
3. Ile kitu 'chilambo cha vene' nasikia mpaka pride fm ya huko mtwara wakaichukua na kuitumia katika kipindi flani. aisee huu wimbo hata mimi unanikosha sana.....bahati mbaya sijaupata
4. Miaka flani ya 2006 hivi nilipita maeneo mengi yanayokaliwa na wamakonde......tandahimba, newala, mtwara, baadhi ya maeneo ya lindi vijijini km vile mtama, litehu, chiuta, mandwanga, mnyambe, lindwandwali, namindondi, mbindo, madingo, malungo, nahukahuka, nyangamara, litipu, linoha, ngunja, mabeti, luagala n.k. sehemu zote hizo walikuwa wanajivunia na kuburudika sana nyimbo za Tongolanga.....nyingi tu (snura n.k)!
Ni mwaka wa nne sasa tangu huyu mwamba afariki 2017😭😭😭😭....wamakonde wote KIMYAAA, kama hakuna lolote lililotokea! nasikia alikuwa anapita vijijini mwenu hata na miguu kuburudisha.
YAANI HAMTAKI HATA KUITANA HAPO DAR (MLIPOJAA KIBAO) MKAANDAA SIKU YA KUMBUKIZI YAKE NA ANGALAU MKAMUONE TU HUYO MAMA YAKE AMBAYE NASIKIA ANA HALI NGUMU SANA MKAMFARIJI?!!!!
nyie wamakonde, nyie wamakonde...........shauri yenu!!!!!
nb:
mwenye chilambo cha vene atupie humu tafadhali