Wamanyema we Tabora me siasa za ukombozi we Tanganyika

Wamanyema we Tabora me siasa za ukombozi we Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WAMANYEMA WA TABORA NA SIASA ZA UKOMBOZI WA TANGANYIKA


1566216675429.png

Abdallah Said Kassongo
Baada ya kusoma historia ya Bi. Dharura bint Abdulrahman msomaji wangu mwingine ameniandikia:

''Asalam Aleykum. Ukitaka khabari za huyu mama nenda nyumbani kwetu Kipata kwa.mama yangu.

Uliza Binti Chamng'anda atakufahamisha zaidi kuhusu huyu mama.

Ni kweli alikuwa mtaa unaitwa Ngoma Circus na pale kulikuwa na mti mkubwa (Mbira) na ofisi ya TANU kwa kumbu kumbu zangu za utotoni zilikuwa pale.

Kama.unaweza kumpata Hasina Kawawa pia lazima awe anamjua ingawa tulikiwa wadogo.

Tabora ilipigania sana uhuru kama hao Mzee Waikela, Mzee Kasongo, Jaafar Kasongo, Ramadhani (Bedui) Singo, Fundi Muhindi, Mzee Mangiringiri, Babu yangu Mzee Chamng'anda na wengine wengi!''

Nami nikamwandikia:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Msukumo wa kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka Combine Dancing Club, club ya vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha.

1566216867548.png

Maulid Kivuruga
Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamng’anda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama.

Wanachama wengi wa kilabu hii walikuwa Wamanyema wa kizazi cha pili baba zao wakiwa wametokea ile iliyokuwa wakati huo ikijulikana kama Belgian Congo, wakafanya maskani Kigoma, Ujiji na Tabora mwishoni mwa miaka ya 1900.

Wamanyema likiwa kabila la Waislam watupu lilijenga namna ya udugu wa kipekee si rahisi kuukuta katika makabila mengine ya mchanganyiko wa dini. Kwao ilikuwa rahisi kuungana kama kikundi cha kabila moja na kuanzisha chama cha siasa kitu ambacho kwa wakti ule kilikuwa cha hatari.

Combine Dancing Club kidogo kidogo ilijigeuza kutoka chama cha starehe na kuwa chama cha siasa.

Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya club ile iliundwa mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu.

Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association New Street, Dar es Salaam kuujulisha uongozi kuhusu ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (Katibu), Chamng’anda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

African Association, kama ilivyokuwa asili ya club iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema.

Hivi ndivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Julius Nyerere, wakati huo akifundisha St. Maryís School, alihudhuria sherehe za uzinduzi wa African Association lakini alikuwa kama mtazamaji tu kwani hakujihusisha na lolote katika chama kile.

Nyerere hakutambua hata kidogo wakati ule kuwa alikuwa akishuhudia sehemu ya historia yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake.

Mwaka 1946 wasomi wa Makerere walianza kujishughulisha na siasa na hivyo na African Association pale Hamza Mwapachu na Julius Nyerere walipochaguliwa Katibu na Katibu Msaidizi na nafasi nyingine za uongozi zikishikwa na wenyewe Wamanyema.

Baada ya uhamisho wa Mwapachu kutoka Tabora, Nyerere akashika nafasi yake na kuwa katibu wa chama.

Mwaka huo huo Nyerere alisafiri kwenda Dar es Salaam kama mjumbe wa Tabora kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa African Association.

Katika mkutano huu ndiyo kwa mara ya kwanza Dossa Aziz alimtia Nyerere machoni.

Lakini urafiki baina ya Dossa na Nyerere haukushamiri hadi mwaka 1952, Nyerere alipokuja Dar es Salaam na kujuana na Abdulwahid Sykes.''

Picha:Abdallah Said Kassongo na Maulid Kivuruga.
 
Back
Top Bottom