#COVID19 Wamarekani 1000 wafa kwa corona ndani ya siku moja tu

#COVID19 Wamarekani 1000 wafa kwa corona ndani ya siku moja tu

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Zaidi ya Wamarekani 1,000 wengine wapoteza maisha kwa corona kwa siku moja.

Takwimu mpya zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha nchini Marekani zinaonesha kuwa, zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha katika kipindi cha masaa 24 na kufanya idadi ya Wamarekani waliokufa hadi hivi sasa kwa ugonjwa huo kuwa zaidi ya 606,179.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, takwimu mpya za wagonjwa wa COVID-19 zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Hopkins cha Marekani zinaonesha kuwa, hadi hivi sasa Wamarekani milioni 33 na 971,207 wameshathibitishwa kukumbwa na ugonjwa huo. Kati ya hao, zaidi ya laki sita na 6,179 wameshafariki dunia baada ya zaidi ya watu 1,006 wengine kufariki dunia katika kipindi cha siku moja.

Kwa mujibu wa tovuti ya "Worldometers" inayotoa takwimu mubashara za corona duniani, hadi hivi sasa watu milioni 169 na 121,221 wameshathibitishwa kukumbwa na COVID-19 kote duniani. Kati ya hao watu milioni 3 na 513,583 wameshafariki dunia na milioni 150 na 770,610 wameshapata afueni.

Marekani imeathiriwa vibaya na COVID-19 kutokana na uzembe.

Marekani ndiyo inayoendelea kuongoza kwa mbali dunia kwa idadi kubwa ya watu waliokumbwa na corona na kufariki duniani kwa ugonjwa huo ikifuatiwa na India, Brazil na Ufaransa.

Huku hayo yakiripotiwa, hivi karibuni afisa mmoja wa masuala ya takwimu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema kuwa, idadi halisi ya watu wanaoaga dunia kutokana na kirusi cha corona ni mara tatu zaidi ya ile inayotangazwa.

Dk Samira Asma, mbaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia alisema kuwa, takwimu za idadi halisi ya watu walioaga dunia kwa maradhi ya COVID-19 inakadiriwa kuwa baina ya watu milioni 6 hadi 8.
 
Si kuna chanjo huko lakini inakuaje tena? Anyways ngoja niunde tume ili nisijifungie nikawa niko kama kisiwani.
 
Back
Top Bottom