Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,253
Wamarekani Kuibeba Soka Ya Tanzania
Na Jessca Nangawe
MAKAMU wa Rais wa Chama cha Soka Marekani cha The New England Revolution, Craig Tornberg amewasili nchini kwa lengo la kutengeneza mahusiano na ushirikiano katika soka baina ya Tanzania na Marekani.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF, Fredrick Mwakalebela alisema wadau hao wa soka wamekuja nchini kwa lengo la kuendeleza mchezo wa soka pamoja na kubadilishana mambo mbalimbali katika soka ikiwa ni sehemu ya kubadilisha uzoefu.
Alisema tayari wamekutana na viongozi wa serikali pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ambapo wamekubaliana kushirikiana katika mpango huo kukuza soka ya Tanzania ikiwa ni kupeleka baadhi ya wachezaji wa hapa nchini Marekani kucheza michezo ya kirafiki.
Mwakalebela alisema baadhi ya viongozi kutoka Wizarani wataondoka nchini Novemba 15 kwenda Marekani lengo likiwa kupata uzoefu na kuangalia viwanja vitakavyotumika katika michezo mbalimbali itakayochezwa huko.
"Tumekubali kushiriki mpango huu kwani kwetu utakuwa na umuhimu mkubwa kwa kupandisha soka letu na kutakuwa na majaribio kwa wachezaji wetu kabla ya kuon doka kwenda huko vilevile wachezaji wa huko watakuja huku ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika mpira,"Alisema Mwakalebela.
Naye Craig Tornberg alisema wamekuja Tanzania kwa kutengeneza mahusiano mazuri ya kimichezo na timu za Tanzania na lengo kubwa ni kupanua wigo wa kimichezo kwa nchi za Afrika hasa kwa vijana wenye umri mdogo ili kuwaandaa kuja kuwa wachezaji wakubwa kama zilivyo nchi za Ulaya.
Timu zitakazoshiriki katika mpango huo ni timu ya taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu pamoja na timu za vijana.
Mwananchi Read News