Wamarekani wamekuwa obsessed na app za mchina sasa

Wamarekani wamekuwa obsessed na app za mchina sasa

def_xcode

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,896
Reaction score
5,181
Zimebaki siku tano hadi ban ya tiktok kuanza nchini Marekani lakini habari zinasema japo tiktok inajaribu kuwapeleka watuamiaji wake kwenye app yao nyingine inayoitwa lemonde wao wameamua kuanza kutumia app nyingine ya mchina inaitwa rednote ambayo ni kama mchanganyiko wa instagram, reddit na shopping.

Habari inasema kuwa watumiaji wa tiktok wanahamia huko kwa maelfu wakijiita kuwa ni tiktok refugees.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba, bora tiktok ilikuwa imeamua kutengeneza kitengo cha tiktok kinachojitegemea wka soko la marekani, lakini rednote ni app ambayo kila kitu chake kiko china na wamarekani hawajali sijui masuala ya national security wala data zao kuwa china.

Na hii si mara ya kwanza maana kuna app nyingine ya shopping ya mchina ambayo inakuja kwa kasi marekani.

Hili linaonyesha kuwa, kama marekani na ulaya isingepiga ban magari na bidhaa nyingine za mchina, generation Z hawajali wangezinunua kwa kasi ya 5G.

Imefika wakati sasa america badala ya kutumia sana ban iongeze ubunifu maana bans haziwezi kutatua wimbi la mcina linalokuja in the long run.
 
Wewe haujui wachina wewe

Unawajua tu kwa chaneli ya kicks

Wala hata haujui vitu gani vya asili ya US ambavyo viko limited and banned hapo US.

So hatua ambayo US anachukua ni bora sanaaaaa. Hongera kwao
 
Wewe haujui wachina wewe

Unawajua tu kwa chaneli ya kicks

Wala hata haujui vitu gani vya asili ya US ambavyo viko limited and banned hapo US.

So hatua ambayo US anachukua ni bora sanaaaaa. Hongera kwao
Najua sana karibu apps zote za US hazifanyi kazi china labda kwa vpn.
Point ya msingi hapa ni kwamba, zamani kanuni za UI zilikuwa zinasema kwamba minimalism ndiyo inayofanya kazi kwa west kwenye app design. Hii ndiyo maana ulikuwa unaona app za west zinakuwa hazina vitu vingi ndani yake yani simplicity.
Mchina yeye, app zake zilikuwa zinahusisha vitu vingi na ndiyo maana hata alibaba kulikuwa na app ya china ambayo ilikuwa na mambo mengi na app kwa ajili ya rest of the world ilikuwa na simplicity.
Sasa mambo yamebadilika, it seems hata west now wako obsessed na super apps kama wechat, kama hiyo rednote yani app moja ina mambo mengi ndani yake. Elon lengo lake ilikuwa ni kuigeuza twitter iwe super app kama ilivyokuwa wechat sijui hadi sasa kafikia wapi.
So, point hapa ni kwamba ban hazitasaidia sana kwa muda mrefu bali trend ya innovations na principles zinabadilika. Hiki kizazi kiko interested na vitu tofauti ndiyo maana tiktok na app za kichina zinaonekana zinawavutia zaidi. waongeze ubunifu kuliko ban.
 
Hii ni vita ya kibiashara, rejea issue ya HUAWEI
Ndiyo maana nikasema ban hazifanyi kazi. Ban kwa huawei badala ya kuiua zimeifanya iwe stronger than ever. Now wanatengeneza chips zao na wamewekeza sana kwenye kuzalisha chips. So akaweka vikwazo wasiuziwe modern Lithography machines ili asiweze kutengeneza modern chips.
Ila mchina now kajikita kwenye research na kujaribu sasa kutengeneza machines na njia zake za kuzalisha chips bora zaidi. Baada ya miaka akdhaa atakuja kushutka jamaa wanazalisha chips na machine za kutengeneza hizo chips wenyewe.
So ban sasa haisadii sana in the long run.
 
Apps ngapi za US zinafanya kazi China?

Whatsapp, google, twitter, IG zinapatikana China?

Hii ni retaliation tu mchina ndo alianza. Tiktok itaendelea kufanya kazi hawa wamarekani wanataka mgao wao tu, taifa huru hili. Washakutana na Trump na Elon huko.
 
Kunya anye kuku akinya bata kaharisha.

China Kublock app sawa ila Marekani aaah
 
Apps ngapi za US zinafanya kazi China?

Whatsapp, google, twitter, IG zinapatikana China?

Hii ni retaliation tu mchina ndo alianza. Tiktok itaendelea kufanya kazi hawa wamarekani wanataka mgao wao tu, taifa huru hili. Washakutana na Trump na Elon huko.
Sio retaliation ni vita ya kiuchumi. Mmarekani hakuwahi kufikiria kuwa watu wake wanaweza kuwa obsessed na apps za kichina maana karibu apps zote maarufu za social media na shopping duniani ni za Wamarekani.
But ndiyo hivyo labda azifungie zote generation Z ya marekani iko obsessed nazo ndiyo maana unaona Elon anataka kutengeneza app kama WeChat, yani super app.
 
Sio retaliation ni vita ya kiuchumi. Mmarekani hakuwahi kufikiria kuwa watu wake wanaweza kuwa obsessed na apps za kichina maana karibu apps zote maarufu za social media na shopping duniani ni za Wamarekani.
But ndiyo hivyo labda azifungie zote generation Z ya marekani iko obsessed nazo ndiyo maana unaona Elon anataka kutengeneza app kama WeChat, yani super app.

Vita ya kiuchumi by retaliation au apps za US zinafanya kazi China? y/n
 
Vita ya kiuchumi by retaliation au apps za US zinafanya kazi China? y/n
Hazifanyi na si kitu ambacho kimeanza leo. It has always been like that.
Lakini ban ya bidhaa za China US kwa sasa ni almost kila kitu. Ana ban kila bidhaa inayofanya vizuri kwenye soko lake, na hauzi anaban kila teknolojia itakayomfanya aweze kutengeneza vitu vizuri zaidi. Hivyo si kwamba ni retaliation ya apps zake kutokufanya kwake, maana asingeweka ban ya magari ya mchina kuuza US, asingeweka ban ya Huawei ndani ya US, asingeweka ban ya makampuni kama Nvidia kuuza graphics cards china.
Hii ni vita ya kibiashara. Sasa ameenda mbali zaidi juzi kaweka vikwazo kiasi kwamba ni kama vile Nvidia inaweza kuuza chips za AI kwa nchi 18 tu maana anadai nchi nyingine zinanunnua then mchina anazichukua huko, CEO wa Nvidia anasema hiyo ban inaenda kuua biashara yao maana ni kama vile watapoteza 90% ya mauzo.
Same to Europe na ban ya EVs za mchina. Car makers wa Germany wanadai mchina akiweka ban ya magari yao basi watapata hasara zaidi.
Hii ni vita ya kiuchumi wala si retaliation.
 
Back
Top Bottom