Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

Wamarekani wanamuhitaji Donald Trump sasa kuliko walivyomuhitaji mwaka 2016

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2016, na kuingia Ikulu 20/01/2017 baada ya kula kiapo.

Katika kipindi cha uongozi wake, alifanya mengi, yakiwemo yaliyowafurahisha na yaliyowakwaza Wamarekani.

Ingawa alionesha chuki kwa baadhi ya Mataifa, hasa ya Kiafrika, lakini alilifaa sana Taifa lake la Marekani.

Mwaka huu Wamarekani watapiga kura ya kumchagua Rais.

Bila shaka, wengi wanajua kuwa wanamuhitaji sana Trump kuliko wakati mwingine wowote.

Uthubutu wake utawezesha vita vya Urusi na Ukraine kufikia ukomo. Anaweza kusaidia kuleta amani Mashariki ya Kati, japo itakuwa ni kwa muda tu.

Atamdhibiti Rais wa Korea Kaskazini asiwe tishio kwa Marekani na maslahi ya Marekani.

Japo si nabii, lakini naamini Trump atashinda Kiti cha Urais wa Marekani mwaka huu

Hata Wamarekani waliomo humu JF, japo ni wachache, lakini wanalijua hilo.

Hawatafanya kosa. Wameamua kwenda na bilionea Donald Trump.
 
Sio rahisi kushinda

Anaandaliwa mazingira ya kushindwa kimfumo toka alipoondolewa ikulu
 
Zelensky nguvu moja umetusaidia kumfanya putin awe uchi
 
Back
Top Bottom