PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
wawakilishi kutoka Kata za Enduleni, Kakesio, Aleilai, Alaitole, Nainokanoka, Olbalbal, Misigyo, Engaresero, Olorieni na Kata ya Ngorongoro.
Akizungumzia uhitaji huo, mwakilishi wa wananchi wa Kata ya Endulen, Foibe Lukumay, alisema wananchi hao, hasa wa jamii ya kifugaji ya Kimasai wanatamani kuondoka Ngorongoro na kwenda kwenye makazi mapya ili wakaanze shughuli za kiuchumi kwa uhuru na upana zaidi.
“Nimeamua kuhama kwa hiari yangu japokuwa napata vitisho katika eneo ambalo ninaishi hasa kutoka kwa viongozi, ndio maana wengi hawataki kuhama.
‘Hata sasa, mimi nimepata vitisho kama Mjumbe wa Serikali ya Kijiji, kama Makamu Mwenyekiti Baraza la Wazee wa CCM wa Wilaya ya Ngorongoro, lakini nikaamua kwa hayo yote niondoke kwa hiari ili tuweze kuinusuru Ngorongoro.
Wanyamapori waweze kuwapo maana wameongezeka kwa kweli. Wameongezeka maana mpaka hata kwangu, wanalala mpaka hapo nje.”
Mwakilishi mwingine wa Kata ya Olbalbal, Christopher Oloju, alisema ameona ni vyema aondoke eneo hilo ili kuitikia wito wa serikali kama ilivyoelekeza.
“Nimekubaliana na baadhi ya familia yangu, ila suala la kufika kule na kuona eneo ni jambo zuri. Nikifika pale (Msomera), hata ile familia yangu nitawahamasisha kuhama.
Mahali popote unapoenda ni vyema uelewe kwanza unapokwenda, ukaona kwa macho na kujiridhisha na kuona maendeleo yanayoelezwa.
View attachment 2174920View attachment 2174921View attachment 2174924View attachment 2174922View attachment 2174923View attachment 2174925View attachment 2174926View attachment 2174927