Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Wote tunatambua kuwa wamasai wa Ngorongoro wamehamishwa toka makazi yao ya asili huko Mkoani Arusha, wakavushwa mkoa wa Kilimanjaro, mpaka kwenda kutupwa mkoani Tanga. Huu ni uharamia mkubwa dhidi ya utu ambao haujawahi kutokea.
Mara kadhaa watu wamehamishwa kupisha miradi mbalimbali. Na katika kufanya hayo, sheria ya ardhi na fidia hutumika. Na uhamishaji unaweza kuwa wa hiari au wa lazima. Lakini kwa hali zote mbili, anayehamishwa huwa haitegemewi kupelekwa umbali wa zaidi ya kilometa 20. Na hata gharama ya kumhamisha mhusika pamoja na mali zake, huzingatia umbali usiozidi kilometa 20. Ndani ya umbali huo huwa haitarajiwi aliyehamishwa kukutana na mazingira tofauti sana na yale aliyokuwa ameyazoea.
Mwanadamu anapoishi, mazingira yake humfundisha mambo mengi, na hivyo mhusika hujijengea uelewa mkubwa wa namna ya kukabiliana na mazingira yake yanayomzunguka. Ni uzoefu na elimu hiyo ya mazingira aliyokulia ndiyo humfanya atambue alime mazao ya namna gani na wakati gani, afuge mifugo ya namna gani na kwa namna gani, ajenge nyumba za namna gani na kwa namna gani, afanye nini na aishi kwa namna gani ili kujiepusha na maradhi ya aina fulani, n.k. Hapa naongelea mwananchi wa kawaida kabisa ambaye kuyamudu mazingira yake hategemei elimu ya darasani wala utajiri wa fedha na zana mbalimbali za tekinolojia ya kisasa.
Lakini leo tuna wamasai waliohamishwa toka mazingira yao ya asili, na kupelekwa mbali kabisa, wakivushwa mkoa mmoja katikati (Kilimanjaro) mpaka Tanga. Yaani wakaanze kujifunza kuyaelewa mazingira mapya, na kisha kujenga uwezo wa kukabiliana na hayo mazingira mapya.
Mbaya zaidi, kitendo hiki ni sawa na kufuta kabisa asili, historia yao na kuwatenga kabisa na jamii zao za asili zilizosalia maeneo ya huko Arusha.
La kusikitisha zaidi, watawala hawa wasio na upendo wala uzalendo kwa Taifa, wanayafanya haya yote ili kumnufaisha na kumfurahisha mwarabu mmoja anayetajwa kuwa eti ni mwekezaji kwenye mbuga ya wanyama ya Ngorongoro huku jamii nzima ya wamasai ikipuuzwa dhidi ya matakwa ya mwarabu!
Tujiulize, huyo Mwarabu hapo Ngorongoro, amewekeza nini? Ameleta fisi, pundamilia, twiga na simba toka Uarabuni? Ameleta ardhi au nyasi wanazokula wanyama pori toka Uarabuni? Kwa nini watawala wanawafanya wananchi hawana akili kiasi hiki? Kwa nini wavunaji na wanufaika wa rasilimali asilia kama wanyama na misitu, wanaitwa wawekezaji?
Hakika wamasai na Watanzania wote, tukiichagua tena CCM au kuwakubalia waendelee kubakia madarakani kwa njia zao zile walizozoea, za uporaji wa kura au kuwatangaza ambao wananchi hawakuwachagua,, nasi tutakuwa na haki ya kulaanika, sawa na wale waliowatendea uovu wale wamasai waliofurushwa kutoka maeneo yao asili ili kutii mataka ya mwarabu mnufaika wa rasilimali za Tanganyika.