Wamasai waandamana katika ubalozi wa Kenya kuiomba serikali ya Kenya kuingilia kati upotoshaji wa zoezi linaloendelea la Loliondo na Ngorongoro

Maryam Malya

Senior Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
116
Reaction score
260
Wamaasai kutoka maeneo mbalimbali wamefanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya Tanzania, uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam leo juni 17, 2022 kuiomba serikali ya Kenya iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wanaharakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya Ngorongoro pamoja na tarafa ya Loliondo.

Wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya wamaasai na serikali ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.

Hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na katibu wa umoja huo anayetambulika kwa jina la loishiye lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la emanuel.

Hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo.
 
WAMAASAI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WAMEFANYA MAANDAMANO YA AMANI HADI UBALOZI WA KENYA TANZANIA, ULIOPO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM LEO JUNI 17, 2022 KUIOMBA SERIKALI YA KENYA IINGILIE KATI UPOTOSHAJI UNAOFANYWA NA ASASI ZA KIRAIA NA WANAHARAKATI KATIKA ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LINALOENDELEA KATIKA WILAYA YA NGORONGORO PAMOJA NA TARAFA YA LOLIONDO.
.
Ngoja watakaokerwa na hili waje...

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama ni Kenya, si waandamane tu, sisi hatuna shida nao, ila Ngorongoro and Loliondo lazima waondoke Wakenya nyang'au sana, wamejaza wamasai wao na mifugo yao Tanzania, sbb Kenya hakuna malisho, alafu wanaandamana huko Kenya, waache waandamane tu.
 
WAMAASAI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WAMEFANYA MAANDAMANO YA AMANI HADI UBALOZI WA KENYA TANZANIA, ULIOPO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM LEO JUNI 17, 2022 KUIOMBA SERIKALI YA KENYA IINGILIE KATI UPOTOSHAJI UNAOFANYWA NA
Hivi siku hizi Tanzania maandamano yana ruhusiwa? Au intelijensia ya Siro haikufanya kazi leo?
Naona ina tumika nguvu kubwa sana kwenye hii issue ya kuwaondoa Wamaasai kwenye makazi yao.
Mimi naamini haya maandamano yame andaliwa na kitengo cha propaganda ili kuuhadaa ulimwengu.
 
Hivi vikundi vinavyojiita vya wamasai vinatengenezwa tu, havina maana wala yale wanayofanya hayana maana, ni siasa tu.

Uvunjifu wa haki za binadamu hauwezi kuvumiliwa popote hapa duniani, na hili haliwezi kuhusiana na kuingilia haki za taifa lingine, Tanzania sio kisiwa.

Muhimu Ngorongoro isitolewe bure kwa mjomba.
 
Propaganda!

Tanzania ina inferiority complex sana kwa Kenya sijui ni kwa nini ? Kwa nini hatujiamini na kutatua matatizo yetu badala ya kutafuta kulaumu kila mtu na kila kitu ? Tunajishusha sana!
Kama ni kweli basi ni wachache waliosombwa na kupekwa hapo baada ya kupewa malipo. Ni ujinga uliopitiliza.
 
Wamaasai kutoka maeneo mbalimbali wamefanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya Tanzania, uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam leo juni 17, 2022 kuiomba serikali ya Kenya iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wanaharakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya Ngorongoro pamoja na tarafa ya Loliondo.

Wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya wamaasai na serikali ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.

Hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na katibu wa umoja huo anayetambulika kwa jina la loishiye lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la emanuel.

Hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo.
Leo wana intelejensia walikuwa wapi??
Au Dunia ishavaa sketi!?
 
Propaganda!

Tanzania ina inferiority complex sana kwa Kenya sijui ni kwa nini ? Kwa nini hatujiamini na kutatua matatizo yetu badala ya kutafuta kulaumu kila mtu na kila kitu ? Tunajishusha sana!
Kwani harakati zinazoendelea huko Kenya kuhusu zoezi la kuwahamisha wamasai kutoka ngorongoro huzioni!?
Wakenye hawajawahi kuwa wema kwa Watanzania.
 
Wamasai wa Ngorongoro wasilazimishwe kuhamia Handeni na badala yake wapewe fidia wajiamulie wapi pa kujaga(kwenda)
Sidhani kama wamelazimishwa mkuu, pia nadhani hata walipewa muda wa kuondoka wenyewe. Sijasikia mtu kukamatwa kwa nguvu kupelekwa Handeni.
 
Kwani harakati zinazoendelea huko Kenya kuhusu zoezi la kuwahamisha wamasai kutoka ngorongoro huzioni!?
Wakenye hawajawahi kuwa wema kwa Watanzania.
Nchi yetu tumelala usingizi muda mrefu sana tukipiga siasa tuuu, wenzetu wanalisha ngombe zao kwetu halafu maziwa wanatuuzia gharama ya juu wanavyotaka. Enough is enough! serikali ifanye utaratibu mzuuri kabisa wa hata kuhakikisha kuwa wamasai wa kitanzania wanapatiwa NIN kistaarabu kabisa. La sivyo nchi itaendelea kuliwa na hawa mchwa.
 
Wamaasai kutoka maeneo mbalimbali wamefanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya Tanzania, uliopo Oysterbay jijini Dar es Salaam leo juni 17, 2022 kuiomba serikali ya Kenya iingilie kati upotoshaji unaofanywa na asasi za kiraia na wanaharakati katika zoezi la kuhama kwa hiari linaloendelea katika wilaya ya Ngorongoro pamoja na tarafa ya Loliondo.

Wamasai hao wameeleza kuwa upotoshaji huo umelenga kuichonganisha jamii ya wamaasai na serikali ya Tanzania, pamoja na kuzorotesha jitihada mbalimbali za makubaliano zilizofikiwa na pande zote mbili.

Hayo yameelezwa kupitia barua ya pamoja iliyosainiwa na katibu wa umoja huo anayetambulika kwa jina la loishiye lashilunye iliyosomwa na kiongozi wa msafara aliyejitambulisha kwa jina moja la emanuel.

Hatua hii inakuja baada ya zoezi la kuweka alama za mipaka katika eneo la loliondo pamoja na uhamaji wa wananchi wa ngorongoro ambapo licha ya serikali kutanabaisha uwepo wa makazi mapya katika eneo la handeni, kumetokea upotoshaji na uchochezi unaolenga kukwamisha zoezi hilo.
Endeleeni kuwavisha mashuka mekundu wasela ili wajulikane kama wamasai
 
Nchi hii inalaana vijana na wazee hadi Sasa mnafanya propaganda za Karl Peter's hatutaweza kuendelea Kwa chama kama CCM
 
Kwani harakati zinazoendelea huko Kenya kuhusu zoezi la kuwahamisha wamasai kutoka ngorongoro huzioni!?
Wakenye hawajawahi kuwa wema kwa Watanzania.

Aha, unajua raisi Samia aliwaomba radhi tena ndani ya Ikulu yetu? Alimpa Uhuru Kenyata Raisi Kenya special treatment huku wakimponda Magufuli, sasa imekuwaje tena?
Mliwaomba radhi kwa “ukatili“ tuliowafanyia kuku wao, sasa kwa nini tena mnaanza kulia kwamba Wakenya wanawahujumu, nilifikiri ni marafiki wa Samia, au ?
 
Back
Top Bottom