Wameishika YouTube robo 3 ya 2021

Wameishika YouTube robo 3 ya 2021

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Ikiwa leo zimebaki siku 90 kumaliza mwaka 2021, ikiwa pia imetimia robo tatu ya mwaka, kuna video nyingi za muziki wa Bongofleva zimefanikiwa kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa kipindi hicho.

Baadhi ya video hizo ni:

1. Sukari - Zuchu

Video ya wimbo huu iliyotoka Januari 30, 2021 ikiongozwa na Kenny tayari imejikusanyia watazamaji milioni 53. Ndio wimbo pekee wa msanii wa kike kutazamwa zaidi Afrika Mashariki.

2. Mbosso - Baikoko

Wimbo huu aliomshirikisha Diamond Platnumz unapatikana kwenye albamu yake ‘Definition of Love’, video yake ilitoka Aprili 9, 2021 ikiongozwa na Kenny, ikiwa na watazamaji milioni 24.7.

3. Harmonize - Attitude

Video ya ngoma hii ambayo Harmonize ameshirikiana na Awilo Longomba na H. Baba ilitoka Aprili 23, 2021 ikiongozwa na Elvis, tayari ina watazamaji milioni 13.4.

Youtube 2

4. Nyumba Ndogo - Zuchu

Ikiwa ni miezi miwili tangu itoke, video hii iliyoongozwa na Hanscana na kuachiwa Julai 1, 2021, tayari imejikusanyia watazamaji milioni 11.9 na kuweka rekodi ya kuwa video ya singeli iliyotazamwa zaidi.

5. Yalah - Mbosso

Ni miongoni mwa nyimbo zinazopatikana kwenye albamu yake ‘Definition of Love’ tena, video yake imeachiwa rasmi Machi 13, 2021 ikiongozwa na Hanscana, hadi sasa ina watazamaji zaidi ya milioni 10.9 tangu iachiwe.

6. IYO - Diamond Platnumz

Licha ya kutangulia na video ya wimbo ‘Kamata’, bado kichupa cha wimbo ‘IYO’ aliowashirikisha Focalistic, Mpara A Jazz na Ntosh Gazi imefanya vizuri, ilitoka Julai 29, 2021 chini ya Hanscana, tayari ina watazamaji zaidi ya milioni 9.8.

7. Kiuno - Rayvanny

Miongoni mwa ngoma zinazopatikana kwenye albamu ‘Sound From Africa’, video yake imetoka Februari 10, 2021, aliyeiongoza ni Kenny, tayari imeweka kibindoni watazamaji zaidi ya milioni 8.4.

8. Jennifa- Rayvanny

Huu ni wimbo wa msanii Guchi kutoka Nigeria, Rayvanny alifanya remix yake na kumshirikisha, video yake iliyosimamiwa na Eris Mzava tayari ina watazamaji milioni 8.0 tangu itoke Julai 9, 2021.

Youtube 1

9. Alikiba - Jealous

Mwimbaji huyu wa Kings Music alifunga safari hadi Lagos, Nigeria kwa mwongozaji muziki Pink na kufanya video ya wimbo huo aliomshirikisha msanii Mayorkun, kutoka nchini humo, video yake ilitoka Julai 30, tayari ina watazamaji milioni 7.7.

10. Sandakalawe - Harmonize

Miezi miwili tangu video hii iliyosimamiwa na Oyin Ameen kuachiwa, tayari ina watazamaji zaidi ya milioni 7.1 tangu kutoka kwake Julai 1, 2021 ukiwa ndio wimbo wa kwanza wa Harmonize wenye mahadhi ya Amapiano.

Youtube 3

Hivyo basi, ni wazi hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2021 wasanii kama Zuchu, Mbosso, Rayvanny na Harmonize wamekuwa na wakati mzuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube, kwani wameweza kuingiza video mbili kwa kila mmoja kwenye orodha hii.

©Mwananchi
 
Harmonize aache nyimbo za dis, akiachana na haya mambo atafika mbali sana.
Watu wanataka burudani, dis peleka kwa waimba taarabu.

Aige mfano wa Diamond na Alikiba. Huwezi sikia sijui kamdis nani. Ni burudani kwa kwenda mbele
Harmonize anazingua sana, sasa hivi huwa sikilizi hata nyimbo zake kbsa, nyimbo za kimbeya mbeya huwa sisikilizi hata kidogo.
Aende akasikilize nyimbo ya Kwangaru, Never give up, na kuna ile nyimbo kamshirika Anjela. Hizi nyimbo kaimba.
Sasa hivi anatoa nyimbo za kipuuzi sana.

Sema ukweli Anjella ana sauti tamu balaa, Zuchu aingii mule.
Hongera Angela. Una sauti tamu ambayo sijaisikia kutoka kwa msanii mwingine wa kike Tanzania
 
Ule wa domo na koffi una ngapi?
 
Back
Top Bottom