Wameshindwa kujitetea suala la DP World sasa wamehamia kwenye udini

Wameshindwa kujitetea suala la DP World sasa wamehamia kwenye udini

Status
Not open for further replies.

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Mimi ni Mkatoliki, nikianzisha mjadala unaopinga Mkataba wa DP World kuhusu Bandari yetu basi naitwa mdini, naambiwa mimi mkatoliki sipendi waislam! Huu ndio ujinga gani?

Yaani mnashindwa kujubu maswali muhimu ya wananchi mnaanza kuita watu ni wadini? By the way mtu ambaye anatafasiri kila tukio kwa hisia za kidini basi huyo ni mdini Namba moja, ni mtu hatari sana.

Sasa nawashauri serikali acheni hizo mtatuharibia Nchi. CCM ya zamani yenye kujibu hoja imefia wapi? Kweli mmeona hili la udini ndio litawanasua?

Hata hivyo wananchi wanaelewa sana. This time wote wameungana. Hiyo ya udini mnaimba ninyi kwa ninyi kwa viitikio mnavyojua nyie.
 
Wamefeli na upuuzi wao, walijua wakigusa dini ndio mwisho wa maswali, wasijue tuko zama mpya kabisa, kizazi cha kuhoji kinachohitaji majibu sahihi, sio propaganda za kijinga.
 
Wamefeli na upuuzi wao, walijua wakigusa dini ndio mwisho wa maswali, wasijue tuko zama mpya kabisa, kizazi cha kuhoji kinachohitaji majibu sahihi, sio propaganda za kijinga.
Mpaka nimewashangaa ni watu wa namna gani.
 
tuambieni yaliyojiri leo kwenye mkutano, wengine tuko mbali, na ni sasa tunaingia humu.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom