"Wamesoma kwa kodi zetu"

"Wamesoma kwa kodi zetu"

Kikongoti

Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
5
Reaction score
0
Sasa hivi kuna uchangiaji katika elimu hasa elimu ya juu. Na kuna baadhi walinyimwa kabisa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kwamba ni watoto wa maskini na wana sifa stahiki za kupata mkopo kwa 100%. Lakini baada ya jitihada binafsi za kujisomesha, baadae unakuja kuambiwa uwe na fadhila maana umesoma kwa kodi zetu (Wa-Tanzania)!

Lakini na hata huyu ambae amesoma kwa mkopo, amesoma kwa kodi za Watanzania au amejisomesha? Maana huu mkopo lazima aurudishe. Hii imekaaje? Kuna uhusiano wa hili 'kujisomesha' na uzalendo?
 
kabla ya 2011 kulikua na Mkopo usio kua na riba, ila baada ya 2010 kuna riba ya 6% so sidhani kama hiyo ni bure!!
 
Sasa hivi kuna uchangiaji katika elimu hasa elimu ya juu. Na kuna baadhi walinyimwa kabisa mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na kwamba ni watoto wa maskini na wana sifa stahiki za kupata mkopo kwa 100%. Lakini baada ya jitihada binafsi za kujisomesha, baadae unakuja kuambiwa uwe na fadhila maana umesoma kwa kodi zetu (Wa-Tanzania)!

Lakini na hata huyu ambae amesoma kwa mkopo, amesoma kwa kodi za Watanzania au amejisomesha? Maana huu mkopo lazima aurudishe. Hii imekaaje? Kuna uhusiano wa hili 'kujisomesha' na uzalendo?

cha ajabu zaidi watanzania wanadhani madaktari wanasomeshwa bure eti hawarudishi mikopo yao hii inanishangaza sana na juzi raisi wetu anasema hivyo hivyo kwenye hotuba yake sasa sijui na hii imekaaje
 
Mazoea mabaya, zamani watu walizoea kusema hivyo lakini wanasahau kwamba mambo yamebadilika na hii mikopo tunailipa baada ya kumaliza elimu husika.
 
Back
Top Bottom