Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Ndugu wananchi, tumefokewa na kuonekana hatuna thamani kwa watawala. Maeneo ambayo ayajawahi kupata maji miaka hamsini tunafokewa kwamba tusipowachagua CCM hatupati maji, miaka yote wamewahi kuyaleta?
Tumefokewa kwa kuonekana Kama wajinga na tusiojua haki yakuchagua kiongozi Bora tukiaminishwa kiongozi Bora anatoka CCM, tusikubali kufundishwa kufikiri.
Wameona haitoshi wametuwekea tume na polisi watuelekeze kwa nguvu Nani tumchague, kwenye SANDUKU la kura polisi na tume hawatatushikia kalamu, tufanye maamuzi sahihi kwenye kale kachumba.
Walituvunjia, wametunyima mafao, wamewaelekeza wabunge tuliokuwa nao wasiguswe hata wasipofanya Jambo kwetu. Tusiwafanyie makosa, dawa ya kaidi ni kuwa mkorofi zaidi yake.
Tuwanyatie, tuwakate warejee uswahilini wajifunze kuishi na watu. Tuwafundishe cheo Ni dhamana
TUKAWAFOKEE KWENYE SANDUKU LA KURA