Wakuu,
Kama unamiliki bodaboda, bajaji na daladala, karibu tujadili changamoto tunazopata kutoka kwa watu tuliowaamini na kuwakabidhi vyombo wasimamie.
Pia kama wewe umewahi kuwa dereva au ni dereva na umekabidhiwa chombo njoo tujadili changamoto tunazokumbana nazo kutoka kwa mabosi.
Nakumbuka kuna kipindi niliwahi kumpa kijana bodaboda, mwanzoni alikuwa analeta kipande vizuri sana, ila baada ya miezi 3 akawa anapitiliza hadi siku 3 akija kuleta analeta ya siku moja, na maneno kibao. Ikabidi niiuze tu maana nilihisi nimenunua ugonjwa.