Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 489
Siku chache zilizopita nilikuwa Jijini Mwanza ambapo niliweza kupata burudani kadha wa kadha kutokana na hali ya hewa niliyoikuta huko ukilinganisha na joto la Jijini hapa Bongo. Lakini pamoja na raha zote hizo, kilichonikela zaidi ni jinsi wenye Bar na Hotel wanavyoendesha biashara zao kwa kuendesha biashara zao kizamani.
Niliweza kuzungukia Bar na Hotel zaidi ya kumi, lakini kila nilipoagiza soda aina ya PEPSI nilielezwa kuwa hawauzi kinywaji hicho ila COCA COLA tu. Nilipojaribu kufanya utafiti nikaambiwa kuwa wamiliki wa Kampuni ya Coca huwa wanagawa viti na ahadi za kuwapa ofa za kreti za soda kila mwezi wamiliki wa bar na hotel husika ili wasiuze soda za kampuni nyingine, Je, katika ulimwengu wa ushindani wa kibiashara tunashindana hivyo? Au ni kulazimisha wateja kunywa hata kile ambacho hawakitaki.
Acheni biashara za kizamani wajameni.
Huu ni ushauri usio na TOZO.