Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kiukweli nawapongeza wamiliki wa jengo hili kuona umuhimu wa kuliboboa jengo ambalo ni la muda mrefu tena limeshaanza kuonyesha ishara mbaya.
Bila shaka wamejifunza pakubwa baada ya kuporomoka kwa jengo la kariakoo na kusababisha vifo kadhaa vya watanzania na hata biashara zao kuharibika.
===================
Wamiliki wa Jengo lililopo mtaa wa Msimbazi na Agrey Kariakoo wameamua kuchukua hatua ya kulishusha/ kulibomoa Jengo lao kwa hiyari yao baada ya kuona jengo hilo limekua chakavu na ni hatarishi kwa matumizi kabla halijadondoka na kuleta athari.
Pia, Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
Warda Adallah Mohammed ambaye ni mmoja wa wasimamizi wa Jengo hilo akizungumza na wahandishi wa habari jioni ya leo amesema kuwa uamuzi huo ulifanyika baada ya kulifanyia utafiti jengo hilo na wataalamu kugundua kuwa linatakiwa kuangushwa na halifai kwa matumizi kwani lina zaidi ya miaka 90 toka kujengwa kwake.