Wamiliki wa mabasi yaendayo mkoani mtwara wanalijua hili?

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,603
Reaction score
489
Kweli Mtwara tumeondokana na zama zile za kusafiri siku mbili hadi tatu, siku hizi Masasi unafika saa 9 au 8.45 mchana. Tunashukuru sana kwa hilo. Ila kuna kero kubwa sana inatusumbua abiria waendao Mkoa huo, kulipia bag suala hili kwa kweli linakera sana sana sana, abiria yeyote akisafiri jamani ni lazima achukue bag, sasa inakuwaje ulipe nauli, halafu ulipie tena na bag? hivi hii ni biashara ya madereva na makondakta au ni ya wamiliki wa mabasi hayo? Na je, wamiliki wa mabasi wanalijua suala hili? hivi ukasalimie nyumbani usichukue hata zawadi? na ukichukua zawadi uwaze nauli, gharama ya zawadi, gharama ya bag!!! tutafika kweli?

Kinachonishangaza zaidi, ukisafiri kwenda mikoa mingine kama Arusha, Dodoma, Tanga na kwingineko hukuti mambo kama haya, hata uchukue bag kubwa kiasi gani hilipi, sasa kwanini taratibu wa usafiri zinatofautiana na mikoa mingine? utaratibu huu ulianzishwa na nani? SUMATRA jamani chonde tusaidieni Mtwara tumechoka kulipia mabag kwa kweli, ni bora watuambie nauli sh 30,000/= lakini nikiwa na bag nisilipe kuliko kulipa nauli sh 25,000/= bag na zawadi zingine sh. 20,000/= inchosha sana na mimi nimechoka na hali hii, vyombo husika vifuatilie suala hili
 
Sijawahi panda ndege, lakini nasikia hata kwenye ndege kuna uzito unaruhusiwa ambapo ukizidi kidogo unalipia, sijui kama ni kweli. Sasa iweje nyie mkamuliwe kwenye mabegi. Kule Mby kuna dogo mmoja alikuwa anatumia begi zuri kusafirishia maharage, kwa hiyo kwenye Coster akawa halipii kifurushi, yawezekana na nyie mnatumia ujanja huo kusafirisha mizigo ya biashara kupeleka Ntwara.

Hata hivyo nawapa pole.
 
asee hiyo kitu niliishangaa sana mwaka 2010 nilielekea huko baada tu ya kufika mbagala ambapo niliona ni kama stand kuu ya kuelekea huko walikuwa wanatoza nauli za mizigo inluding mabegi asee nilikuwa na rasket yangu nayo wakadai nauli. niliwapa jibu rahisi tu kuwa silipi labda kama wana swali la ziada. kiukweli hii hali ni mbaya bt nahis wakaz wa huko washazoea mbona walikuwa wanalipa!
 
Tatizo la wa tz ni ujinga we2 ndio unatuponza,Mi mwezi wa 2,nilikwenda mtwara na basi la maning nice,niligoma nikawambia siwezi lipia begi la kg 10! Sheria ni kama begi linazidi kg 20,utatakiwa kulilipia,na mbona ujinga huo kwenye mabasi ya kwenda mwanza,bk ,musoma,haipo? Mambo mengi ni upumbavu we2,na hata haina haja ya kuwa2pia lawama polisi,wala sumatra,kama abiria mnakuwa na msimamo wa pamoja mtafanikiwa.
 
Umesema vema ndg yangu white wizard, ila ndg yangu ni wangapi wanajua hiyo sheria ya bag kulipiwa likiwa na kilo kuanzia 20? ingawa ignorance of law has no excuse, ila ndio maana tunawaomba sumatra na wamiliki, kwanza je wanalitambua hilo tatizo? na je wanalichukuliaje? Wakati umefika sasa kwa wahusika kuwaelimisha wananchi/abiria wa Mtwara ili wajue sheria hiyo
 
Watafute SUMTRA kaka, hao watakoma tu, kama alivyokuambia madau hapo uzito ni kilo 20. na ukizidi kuna bei yake maalumu kwa kilo na sio mambo ya kukadiria.
 
asilimia kubwa abilia vichwa maji,juzi tu nakuja nachingwea mama kalipa elfu 60 ya mizigo hadi mkaguz wa bus najims akastuka akamuuliza mama kweli ukakubali kumpa mtu elfu 60 na mizigo imeachwa?
 
Back
Top Bottom