Wamiliki wa magari kutembeza magari yao wakiwa wametoa plate number ya mbele

Joined
Jul 28, 2020
Posts
41
Reaction score
51
Nawasalimu wadau

Bila kupoteza muda, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wamiliki wa magari kutembeza magari yao wakiwa wametoa plate number ya mbele na kuziweka ndani, hii hali nimeiona zaidi nikiwa mkoa wa dodoma.

Sasa sijui ndo mageuzi au basi tu ni kupungua kwa usimamizi maana sasa inaanza kuwa ni fasheni. Watu wanaigana kila siku hasa hawa wa subaru na alteza ndo wanazidi kuongezeka.

Au ndo mpaka tamko litoke?

Kweli tutafika tumechoka.
 

Yaani hata hueleweki unaongea nini.

Hujui kuweka Kituo, koma wala Aya.
 
Kwani wee ina kuhusu nini au wapi umeumizwa na watu kutoa Plat namba wakati wa kutengeza magari?

Mtaani kwenu hii ndio kero wakati hapo dodoma ni kambi ya ccm miaka mingi kunamatatizo lukuki.
 
Unaweza kuta ni code ya wauza ngada au mashoga
 
Ni vizuri umenote wanafanya sana watu wa subaru na altezza (gari za michezo). Iko hivi ni kweli wapo wanaoiga hasa wa Altezza, Ila chimbuko la hiyo tabia ni kwa gari zilizokuwa modified zikawekwa front mount intercooler (fmic). Sasa hiyo intercooler mahala inapokaa ukiweka namba plate unakuwa unaiziba na kuipunguzia ufanisi hivyo ni mawili aidha number plate ihamie ndani au ufanye modification kwenye bumper ikae pembeni na sio katikati.
 

Attachments

  • IMG_4324.jpeg
    12.2 KB · Views: 13
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…