Wamiliki wa pikipiki za biashara come this way

Wamiliki wa pikipiki za biashara come this way

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
7,460
Reaction score
4,761
Nawasaliimu wote
natumaini all of you are doing fine kabisaa
Nina kitu nawaomba mnisaidie mwenzenu!!
Nina pikipiki ambayo haina kazi nataka niifanye ya biashara iniingizie kitu kidogo kwa familia nimempata na mwendeshaji kabisa sasa basi nashindwa handler procedure

  1. Namkabidhije huyu bwana hii pikipiki?
  2. Niutaratibu gani niufanye maana kuilaza hapo kwangu ni mbali sana na barabarani nimkabidhije ili iwe anaamkia nayo kazini naandikishanaje nae ,wadhamini,kujua nyumbani kwao nini hasa nifanye nisijeibiwa mali yangu!!
  3. Jinsi yaukusanyaji wa hela yangu daily au weekly basis na range yake ni kiasi gani per day ushauri wako ni muhimu sana kwangu mwana jf na ninaamini kuna wengi wanaoifanya hii biashara hapa dsm nishauri jamani
nakaribisha michango yakinifu yakunijenga pia prons and cons pia nipeni as alert nina pikipiki 1.nataka niongeze ziwe at least 2 ni aina gani ya pikipiki ni nzuri kwa biashara in term of spare parts jamani.

Ni mimi wenu mtiifu Nivea
 
Hii biashara nayo ni pasua kichwa kama ilivyo ya daladala na taxi. Unaweza kupata kijana mwaminifu ila ataharibikia kijiweni kwao, maana mbinu wanazopeana za kuibia mabosi wao ni balaa!

Ila yote tisa, kumi akikisha unampa kijana unayemfahamu na ujue na ndg zake, vinginevyo usishangae akisepa nayo! wakati mwingine wanakudanganya ameibiwa kumbe yeye ndo kapanga wizi huo, yaani ni full usanii!!!
 
Kuhusu makabidhiano,ki2 cha kwanza ni kumjua vizuri huyo unaemkabidhi,upajue kwake,na ikiwezekana kama ana jamaa yake ahusishwe pia,awe kama mdhamini wake.Kingine unaandaa mkataba ambao utaweka makubaliano yenu,kuwa amekubali kuwa amekabidhiwa pikipiki namba... Ambayo ni kwa kufanyia biashara,na kiasi ambacho mtakuwa mmekubaliana kwa siku,kiasi kinategemea na makubaliano ila ni kati ya sh.7000-8000,kwa cku,na vizuri zaidi ni kuleta hesabu kwa wiki,ila cku moja ni yake ya kufanya service,atakuwa anakuletea pesa ya cku 6,na mwambie kama kuna tatizo pikipiki imeharibika asitengeneze tu,bila ya kukupa taarifa,kwani anaweza kuwa analeta uhuni,kuhusu kulaza pikipiki kama umeshamwamini analala nayo tu kwake.Ila biashara hii ina changa moto kubwa,mala nyingi wanaofaidika nayo ni hao madreva,na kuleta hesabu hadi mtafutane!Kwa ushauri wangu kabla hujanunua ya 2,anza kwanza na hiyo moja,ukishaweza kuzikabili hizo changamoto ndio utafute na ya pili,kwani una weza kukutana nazo ukashindwa kuzi overcome ukaamua kuiuza tu,mi yalishanikuta ndio maana nakupa angalizo.aina ya boxer ni imala zaidi japo na bei yake ipo juu. ILA KAMA HUNA UVUMILIVU BIASHARA HII NI PASUA KICHWA.USANII MWINGI.
 
Nawashukuru sana kwakupoteza muda wenu kunishauri naendelea kupokea mawazo yenu
 
Back
Top Bottom