Uchaguzi 2020 Wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari, mbona mmekubali upendeleo huu?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
2,946
Reaction score
2,932
Moja kwa moja kwenye mada.

Nimetafakari sana leo, hasa nilipopitia magazeti ya leo tarehe 16. Sijaona gazeti hata moja lililoripoti tukio la kukataliwa na kuzomewa mteule wa CCM kule Kagera.

Hakuna chombo chochote cha kielectronic kilichoripoti tukio lile. Nikashangaa, wanahabari wamekuwa watumwa hivi.

Je, angezomewa Lipumba, Maalim Seif au Membe visingeripoti?

Duuu! Ama Freemason yupo kazini? Kimyaaa! Kama nchi haina vyombo vya habari na wanahabari!

Ivi hamna namna ya kujitetea hata mkapata uhuru wenu?

Karibuni
 
Ukiujubali upumbavu jua na wewe ni mpumbavu

Ilitakuwa Magazeti kama Habari leo , Uhuru na Yale ya mchumia tumbo msiba ndiyo hiyo habari yaipe uzito.
 
Kumbuka hata Yesu aliwaita waandishi wanafiki so usishangae wanyonata na beat.
 
Huwatakii mema hao waandishi na vyombo vyao wanavyo vitumikia! Kwa sasa wameamua kuishi maisha ya kinafiki ili siku ziende na mkono uende kinywani.

Muangalie mtu kamaDeodatus Balile, Pascal Mayalla, nk. Wanaunga mkono juhudi lakini unaona kabisa nafsi zao zinawasuta.
 
KUWAITA WAPUMBAVU WAFANYAKAZI WA UMA, KISA WAMEACHA KUTANGAZA MATUSI YA MGOMBEA WENU, NIKOSA AMBALO UNATAKIWA UCHUKULIWE HATUA KALI KWA MJIBU WA SHERIA.
 
Leo nimepita kijiwe cha kuuzia magazeti nkamuuliza muuzaji kama kuna Gazeti lenye habari za Lissu kasema leo hakuna ila jana Raia mwema waliandika kidogo na gazeti halikukaa hata nusu saa limenunuliwa lote. Na yeye anawalaumu wamiliki kwa kutoandika ipasavyo habari za TL.Yaani kwa ufupi Gazeti bila TL limedoda.
 
Kumbuka hata Yesu aliwaita waandishi wanafiki so usishangae wanavyonata na beat.
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Nimetafakari sana leo, hasa nilipopitia magazeti ya leo tarehe 16. Sijaona gazeti hata moja lililoripoti tukio la kukataliwa na kuzomewa mteule wa CCM kule Kagera.

Hakuna chombo chochote cha kielectronic kilichoripoti tukio lile. Nikashangaa, wanahabari wamekuwa watumwa hivi.

Je, angezomewa Lipumba, Maalim Seif au Membe visingeripoti?

Duuu! Ama Freemason yupo kazini? Kimyaaa! Kama nchi haina vyombo vya habari na wanahabari!

Ivi hamna namna ya kujitetea hata mkapata uhuru wenu?

Karibuni
Haya ndio madhara ya udikteta jamani tukatae mambo haya sasa.
 
Nayaona yamedoda kwenye meza tu...watu wanapita na kuchungulia vichwa vya habari then wanasepa ni makada wachache wanaonunua magazeti.

Back
Top Bottom