nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,946
- 2,932
Haya ndio madhara ya udikteta jamani tukatae mambo haya sasa.Moja kwa moja kwenye mada.
Nimetafakari sana leo, hasa nilipopitia magazeti ya leo tarehe 16. Sijaona gazeti hata moja lililoripoti tukio la kukataliwa na kuzomewa mteule wa CCM kule Kagera.
Hakuna chombo chochote cha kielectronic kilichoripoti tukio lile. Nikashangaa, wanahabari wamekuwa watumwa hivi.
Je, angezomewa Lipumba, Maalim Seif au Membe visingeripoti?
Duuu! Ama Freemason yupo kazini? Kimyaaa! Kama nchi haina vyombo vya habari na wanahabari!
Ivi hamna namna ya kujitetea hata mkapata uhuru wenu?
Karibuni
Enzi za Yesu kulikuwa na vyombo vya habari?Kumbuka hata Yesu aliwaita waandishi wanafiki so usishangae wanyonata na beat.
Leo nimepita kijiwe cha kuuzia magazeti nkamuuliza muuzaji kama kuna Gazeti lenye habari za Lissu kasema leo hakuna ila jana Raia mwema waliandika kidogo na gazeti halikukaa hata nusu saa limenunuliwa lote. Na yeye anawalaumu wamiliki kwa kutoandika ipasavyo habari za TL.Yaani kwa ufupi Gazeti bila TL limedoda.