Wamisionari na Mchango wao katika Kukuza Kiswahili

Wamisionari na Mchango wao katika Kukuza Kiswahili

FINDTRUEFAITH

Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
83
Reaction score
86
Habari zenu wadau!

Ni watu wachache tu ndiyo wanaoelewa kwamba Wamisionari walichangia sana katika makuzi ya lugha ya Kiswahili has a Askofu Steer na John Krapf.

Walipokuwa Mombasa mwaka 1844 walipenda wenyeji wa huko wapate Neno LA Mungu kwa lugha yao (Kiswahili cha Kimvita). Walimuomba aliyekuwa Mufti wa Mombasa kipindi hicho Sheikh Ali Mohedin kuwasaidia kutafsiri baadhi ya maneno ya Kiingereza na kuyaweka katika Kiswahili.

Naye alifanya hivyo kwa kuchanganya na maneno ya Kiarabu.

Leo kwenye Biblia ya toleo LA The Union Version 1952 kuna maneno hayo mfano: Kadhi, Idi, Liwali, Thenashara, arabuni, kalibu, huluku, shehe n.k ambayo yaliwalazimu Wamisionari hao kuchapisha pia Kamusi kwa ajili ya kuwasaidia wasomaji kujua maana ya maneno hayo.

Kadhi yake Hakimu, Idi maana yake Sikukuu, Liwali maana yake Mkuu wa Mkoa, Thenashara maana yake kumi na mbili, arabuni maana yake rehani au urithi, kalibu maana yake tanuri la moto, huluku maana yake umba (MTU). Shehe maana yake mzee.

Wengi wamewasema Wamisionari kwamba walikuwa ni mawakala wa Ukoloni huku wakiwa hawajui historia hii.
 
Back
Top Bottom