Wan ndoa sheria ya kuvunga kizazi ya Tanzania wanawake itawamaliza

Wan ndoa sheria ya kuvunga kizazi ya Tanzania wanawake itawamaliza

POSHO MAVYEO

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2011
Posts
371
Reaction score
112
leo katika pita pita yangu sehemu nimekutana na dada mmoja hakiwa na hali ya uzuni sana,
nilipoongea naye kwa kina nikagundua BUNGE letu la jamuuri limekula kwake.

yeye ana matatizo ya kizazi kila mimba hutoka na hospitalini hawajui tatizo ni nini?
ameshapoteza watoto wengi na sasa ni hatari kwa maisha yake, aliongea na dactari amtoe kizazi
lakini doctor akasema hawezi kumfunga kizazi mpaka mumewe naye sign kukubali.

hapo ndipo nilipochoka ina maana kuna watu wanalazimishwa kubeba mimba, tena kuna sheria hakuna kufunga kizazi mpaka ujadiliane na mtu mwingine hata kama maisha yako yako hatarini?

hizo haki za binadamu na ndoa zina kwenda wapi?

huyo dada mumewe hayuko tayari kuvunga kizazi
 
Kwani ni lazima afunge kizazi. Si atumie njia nyingine za kuzuia mimba hata kuchoma sindano maana hiyo haiitaji ruhusa ya third party. Hata mimi siwezi kumshauri mtu afunge kizazi. Kufunga kizazi si kazi ndogo mama yangu alifunga kizazi japo ilikuwa uzeeni alinambiia mwanangu usijaribu. Kuna lots of complications na ni operation kubwa hiyo kwa hiyo haina siri lazima ndugu na jamaa including sijuhi mume atajua.
 
wewe uoni kama hiyo ni ujangiri kutomshirikisha, anyway nadhani hiyo sheria inaweza kula hata huko issue ya uzazi kama una ndoa lazima wawili msaini karatasi
 
Tunaongea na experience si sheria za kwenye karatasi. Sindano unaenda popote wanakudunga huna haja ya kwenda na mumeo. Ndio maana nimesema huyo mdada hata kama ameshindwa kutoa kizazi akachomwe sindano hatapata ujauzito kwa sababu yeye asichotaka si asipate mimba?? Hiyo ni alternative na ni less complicated.

wewe uoni kama hiyo ni ujangiri kutomshirikisha, anyway nadhani hiyo sheria inaweza kula hata huko issue ya uzazi kama una ndoa lazima wawili msaini karatasi
 
Haina haja yakumficha amueleze ukweli na kama mzazi mwenzie hakuharibiki kitu wataelewana,lakini siri sio nzuri.
 
Pole nyingi kwa huyo dada,
nahisi mume wake hataki mkewe afunge kizazi ksb,
bado ana imani kuwa ipo siku hilo tatizo litamwisha mkewe,
anaamini kuwa atashika mimba na kujifungu salama (watafanikiwa mtoto aliye ndoto ya ndoa yao.

Na nadhani anataka kuchukua huo uamuzi wa kufunga ksb amekata tamaa ya kupata ujauzito,
utakaoweza kutengamaa vizuri pasipo kuharibika.
Ya mungu mengi, na mungu uwa hashindwi jambo, lililo muhimu,
aendee kumwomba mungu pia azidishe imani kwake.

Ila kama ina hatarisha afya yake, basi waongee na mumewe vizuri wakubaliane,
ikishindikana, ma dr ,ndugu wa karibu washirikishwe ili waweze kupata mwafaka.

Pole sana.
 
Mpaka anaamua kutaka kutoa kizazi huyo dada inaonesha ameshakata kabisa hata tamaa ya kuishi. Tumaini mbona lipo? alipofikia ni mbali sana hapo bado suluhisho linaweza kupatikana hakuna kinashindikana chini ya jua
 
Uzazi wa mpango una madhara makubwa sana kwa wanawake baasi tu tufanyeje
 
Mpaka anaamua kutaka kutoa kizazi huyo dada inaonesha ameshakata kabisa hata tamaa ya kuishi. Tumaini mbona lipo? alipofikia ni mbali sana hapo bado suluhisho linaweza kupatikana hakuna kinashindikana chini ya jua

tatizo ni kwamba mimba zinatoka sana
 
Back
Top Bottom