Uchaguzi 2020 Wana ACT-Wazalendo wamuandikia Barua Msajili wa Vyama vya Siasa kumwambia Maalim na Zitto wamepoteza sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo

Msajili hawezi kuwafuta uanachama ila katiba yao itawafuta uanachama, ACT wazalendo walitunga hiyo katiba wenyewe.
CCM hii hoja haitawasaidia pambaneni na hali yenu...mlipanda maovu mnavuna maovu
 
Haha Kwahiyo wewe Tatizo lako ni kwanini wameenda kwa msajili hayo ya wao kuvunja hivyo vipengele havina madhara

Wenye mamlaka ya kuitisha mkutano na kuwafuta uongozi ni hao hao kina ZZK kwa akili yako unategemea hao kina ZZK watafanya huo mchakato ndio Maana wanakwenda far

Hao kina ZZK wenyewe wamewahi kuipeleka chadema mahakamani wakati Sheria yao inasema ukikipeleka chama mahakamani unafutwa uanachama

Leo hao kwenda kwa msajili sio sawa

Ila kwa mambo hayo jua tu upinzani imejaa udikteta kama ilivyo kwa CCM (kwa mujibu wenu)

ZZK na wengine kina Kitila walikipeleka chadema mahakamani wakafukizwa tena wakiongozwa na Lissu na wapinzani wakamcheka haswa ooh anatumika na CCM

Leo na yeye ana chama chake anakua mvunja Katiba aliyotengeneza yeye amebeba tabia zile zile za kina Mbowe

Anapelekwa kwa msajili atawafukuza Hao wanachama
 
Sasa hujui haki ikishindwa kupatikana ndani ya chama inapatikana mahakamani?. Au hujui chombo chajuu cha kutoa haki ni mahakama?.

Nabaada yakwenda mahakamani huoni kama alishindwa kesi?.

Kwahio kwa akili yako unaamini msajili anauwezo wakufuta uanachama hao viongozi?.

Kazi yamsajili nikushauri vyama tu kama mlezi wa vyama nakuvisihi vifate katiba zake, lkn hata vikivunja katiba hizo msajili hana uwezo wakumfuta mtu uanachama, au hatua yake kubwa kabisa kimadaraka nikukitutia usajili chama cha siasa jambo ambalo hawezi.
 
Rudia post zangu zote Sijasema post hata Moja kwamba msajili amfute uanachama ZZK au Maalim Seif

Hoja yangu ni wao kuvunja Katiba yao wenyewe
Kwa tafsiri yako unaona ipo Sawa Mkuu
 
Rudia post zangu zote Sijasema post hata Moja kwamba msajili amfute uanachama ZZK au Maalim Seif

Hoja yangu ni wao kuvunja Katiba yao wenyewe
Kwa tafsiri yako unaona ipo Sawa Mkuu
Sasa kama wamevunja, huoni nahao wanaowatuhumu kuvunja nao wanavunja kwa kutokufuata taratibu zachama, kwa nini wasizunguke mikoani kutafuta sign za viongozi wamikoa na wilaya ili akidi itimie yakulazimisha kuitwa kwa Baraza kuu ili liwavue uanachama?. Kwa nn nao waonaenda kinyume nataratibu zao?.
 
Ww mbona hujahoji jiwe kwa uvunjifu wa Katiba ya nchi?!
Ka uvunjifu wa kujenga barabara kila kona na vichochoro nchi nzima? Au avunjifu wa kujenga fly over hapo ubungo ili muwahi kwenda majumbani kwenu na kuondosha visingizio vya foleni huku mkiwa kwa michepuko?
 
Kwanza tukubaliane wamevunja Katiba yao
Na kama wamevunja je Adhabu yake imeandikwa ni nini?

Halafu tujadili hii michakato yako
 
hawa vibaraka tu
 
Kwanza tukubaliane wamevunja Katiba yao
Na kama wamevunja je Adhabu yake imeandikwa ni nini?

Halafu tujadili hii michakato yako
Siwezi nikasema wamevunja huku maalimu Seifu akimjibu Membe alisema kumuunga mkono mgombea anaekubalika ilifanyika ndani ya vikao vya chama. Sasa ili kupata uhalali kuwa kikao kilifanyika au hakikufanyika, ndio inatakiwa zitafutwe signature za walioshiriki kikao hicho wakiside upande ambao wanakubali au kukataa kuwa kikao hakikufanyika. Nasignature hizo zifike robo tatu ya wajumbe wote, Kisha waite Baraza kuu liizimie kuwa nikweli wamevunja katiba.

Siwezi nikaside upande kuwa walivunja au laa, huku Hawa wakisema walivunja ,huku maalimu akisema iliamualiwa navikao halali vya chama.
 
Hakuna cha goli hapo, wakitaka Z'bar iingie katika Chaos wamuengue Maalim Saif dakika hizi ndio utawajua wazanzibar walipoamkia baada ya awamu hii
Mkuu, hamna kitu.

Maalim keshafahamu hiyo.

Mwinyi hayupo pale kwa bahati mbaya ati.

Hii ni mipango endelevu ya CCM kwa Zanzibar.
 
Ka uvunjifu wa kujenga barabara kila kona na vichochoro nchi nzima? Au avunjifu wa kujenga fly over hapo ubungo ili muwahi kwenda majumbani kwenu na kuondosha visingizio vya foleni huku mkiwa kwa michepuko?
Utekaji, utesaji, mauaji, ufisadi wa ununuzi wa wapinzani kwa fedha za walipa kodi, ubambikiziaji kesi zisizo na dhamana kwa wananchi wasio na hatia, nk..
 
Wacha tuone what next!
BM huoni kwamba na wewe na wenzio mmekiuka katiba ya chama chenu na utaratibu kwa kum-adress msajili bila kupitia vikao vya chama chenu?
Msajili wa vyama sio sehemu ya act kwahiyo mtendaji wa act ni KM wenu ambaye mmemruka! Huo ndiyo utaratibu?

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…