Uchaguzi 2020 Wana ACT-Wazalendo wamuandikia Barua Msajili wa Vyama vya Siasa kumwambia Maalim na Zitto wamepoteza sifa za kuwa wanachama wa ACT-Wazalendo

Kusoma katiba ya taasisi yako unayoiongoza unashindwa alafu unataka upewe nchi inayoongozwa kwa mujibu wa katiba huu ni msiba mkubwa
Kwani katiba haisemi mambo kuamliwa na vikao!! Suala la ACT kumsupport Lissu si likiamliwa kwenye vikao ??? Shida iko wapi???

Ccm jueni tu kuwa hizi mbinu zenu zote zilishajulikana na watanzania tangu mwanzoni. Hakuna lolote mtakalofanikiwa na watanzania Tuko kwenye ajenda moja tu, Ni kuwatoa nyie madarakani Tanzania na Zanzibar mwaka huu
 
ACT wanaenda kutengenezewa mgogoro mkubwa kama ule wa CUF ili wahangaike nao kwa miaka mitano mahakamani na wakose utulivu na amini usiamini majibu ya barua hii yatatolewa kwa kasi ya ajabu. Tusubiri tuone mchakamchaka ndio umeanza huo
 
Kosa moja halifanyi Wala kuhalalisha kosa jingine kuwa usahihi, jibuni kwa hoja za katiba ya ACT wazalendo, acheni kukimbilia neno "mbona..."
Ajenda iliyopo mezani saivi ni kuwatoa Ccm madarakani . Sasa nyie wana Ccm mliyojipenyeza ACT rudisheni hela mlizolipwa, hakuna lolote mtakalofanya mwaka huu na litafanikiwa. Watanzania wako serious kweli mwaka huu
 
Uanachama haukomi kwa kuandika barua kwa msajili, bali taratibu za kichama inabidi zifuatwe. Iwapo msajili atafanyia kazi barua hii ni wazi kuwa tutakuwa tumepata ushahidi ya kwamba ofisi ya msajili ni sehemu ya watesi wa upinzani nchini
 
Halafu kama hata campaign hajapiga
Alitaka aendelee kutambulikana kama mgombea wao?
Membe sio mpinzani bali ni mzee muhuni toka ccm, kaenda ACT hana hata mwezi kapewa nafasi ya kugombea urais. Kama ni demokrasia yeye hakustahili kuipata nafasi.
 

Unanifurahisha sana kamanda unaposema Watanzania tumeamua; Watanzania ajenda yetu moja tu....Kama vile wewe ni msemaji wa Watanzania wote. Angalau fyatisha mawanda ya kauli zako iwe Wapinzani tumeamua, makamanda ajenda yetu...Don't be too delusional [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ajenda iliyopo mezani saivi ni kuwatoa Ccm madarakani . Sasa nyie wana Ccm mliyojipenyeza ACT rudisheni hela mlizolipwa, hakuna lolote mtakalofanya mwaka huu na litafanikiwa. Watanzania wako serious kweli mwaka huu
Broo! Nauliza kuwa hao wanachama halali wa ACT wazalendo wamedanganya hizo allegations dhidi ya Maalimu Seifu Sharrif Hamad na Ndugu Zuberi Zitto Luyagwa Kabwe hazipo sawa kwa mjibu wa katiba ya ACT wazalendo?

Unasema ajenda iliyopo Ni kuing'oa CCM madarakani, kwani ili mchakato huu wa kuing'oa CCM madarakani ufanikiwe Ni sharti mvunje kanuni na katiba za vyama vyenu? Je, ni sawa na Ni halali kuvunja katiba ya taasisi?
 
Matumbo war in offing. CCM puppets in action. An opportunity for betraying the hard and long walk to freedom. The NEC guys are all in teeth - broadly smiling.
 
Uanachama haukomi kwa kuandika barua kwa msajili, bali taratibu za kichama inabidi zifuatwe. Iwapo msajili atafanyia kazi barua hii ni wazi kuwa tutakuwa tumepata ushahidi ya kwamba ofisi ya msajili ni sehemu ya watesi wa upinzani nchini
Kazi ya msajili ni kulea vyama pamoja na kusimama katiba ya hivyo vyama
Isikiukwe na mtu yeyote yule
Cafu walipeleka vielelezo vya ukiukaji wa katiba ndani ya chama cha cafu ibara 117
Iliyopelekea Maalim seif kukimbilia Act
Na leo Act wamepeleka vielelezo vya ukiukwaji wa katiba ndani ya Act ibara ya 13 iv kuonyesha Maalim seif ni mweupe katika kusoma na kusimamia katiba na sheria za taasisi
Anaendesha taasisi kibabe zaidi kuliko kufuata kanuni na sheria waliojiwekea wao wenyewe..
 
Halafu kama hata campaign hajapiga
Alitaka aendelee kutambulikana kama mgombea wao?
Si ndio hapo sasa. Ccm walitegemea cdm wataingia mkenge kama wa Lowassa ndio wakamtoa Membe ili ajifanye mpinzani. Naona ACT kwa sababu wanazojua wao wakauvaa huo mkenge. Ndio saa hii nia ovu ya Membe inapoonekana.
 
ACT wanaenda kutengenezewa mgogoro mkubwa kama ule wa CUF ili wahangaike nao kwa miaka mitano mahakamani na wakose utulivu na amini usiamini majibu ya barua hii yatatolewa kwa kasi ya ajabu. Tusubiri tuone mchakamchaka ndio umeanza huo
Sio kutengenezewa Bali viongozi wenyewe mwenyekiti na kiongozi wa chama
Walitunga Katiba wenyewe na waliweka vipengele kadhaa wakiamini watavifuata wao na wanachama wao.
Sasa kwa maslahi yao Binafsi wanapindua pindua Katiba.

Halafu Maalim huu upuuzi wakujiamulia mambo ya ovyo inaonekana ni utamaduni wake
2015 kweli alishinda kwa mujibu wake Ila papara zake zikampeleka kujitangaza Mshindi kakosa vyote
Kazunguka ulaya Huko kaishia kupiga picha ukumbi mtupu kule UN
Akaja na story kibao
 
Baadhi yenu humu huwa mnalalamika kuwa viongozi wa serikali hawafuati Sheria na katiba, kwanini katika hili mmebaki kulalamika na kuitukana CCM mkiamini kuwa ndiyo imewatuma hao wanachama wa ACT wazalendo ( walalamikaji)?

Kwani madai haya hayapo kikatiba ( ACT wazalendo)?

Kwa mwenendo huu, nawaomba tuacheni kutoa vibanzi machoni pa wengine ilihali sisi tuna boriti machoni petu.

Upinzani wa namna hii unatia mashaka hasa unapoingia kwenye michakato na harakati bila kuzingatia kanuni, Sheria na katiba za vyama husika.......this is a BIG Nooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…