Ndungu zangu wana JF,St. Mathew Secondary ni moja ya shule zilizo na sifa kubwa jijini Dar es salaam lakini vilevile ni shule ambayo ina mafisadi kupita kiasi kwa wale wenye ndugu zao wanosoma pale wanalitambua hilo. Imagine mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne au cha sita anaambiwa atoe Tsh. 10,000 ndo aweze kupata cheti eti kwa madai ya kwamba wamewatunzia vyeti vyao so inabidi wachangie hela ya usumbufu. Sijawahi kusikia jambo kama hili mahali popote pale labda wana JF wenzangu mnipe mawazo yenu kuhusu hili na tufanyeje ili kukomesha jambo hili lisitokee tena..