Wana JF mna roho nzuri sana, naomba mnipokee

Wana JF mna roho nzuri sana, naomba mnipokee

Joined
Jun 16, 2019
Posts
14
Reaction score
18
Ni mara yangu ya kwanza kujiunga na JF wala sina wasi wasi yoyote najua wanajukwaa ni watu wastaarabu na wakarimu hivyo mtanionyesha ushirikiano wa hali na mali.

Sina mengi ya kusema ila naamini kwa hayo machache mtanipokea na kunitambua kama mwanajukwaa mwenzenu. Je wangapi mko tayari kunipokea mimi kama mwana JF mwenzenu?? Ningependa kusikia mrejesho wenu juu ya ombi langu.
 
Jf Kama Dar tu ilivyo. Kuna ushuani na uswazini, Kuna vichochoro hadi fly over, Kuna wasomi na makanjanja, Kuna haters na lovers, Kuna walio real na fake. Kuna watakaokujua kuliko unavyojijua bila kuwasahau mahakimu wa comments na michango yako, usijisikie vibaya wakija fukua makaburi yako
 
Worry not mkuu l will respond to all with love, kindness and respect. But asante kwa ushauri pia.
 
Nimekuja kujumuika kama mwana JF kwa lengo la kujifunza, kupata ushauri, ujuzi na maarifa, marafiki wapya, kushiriki mijadala ya hapa jukwaani na mambo mengine kadha wa kadha kama itakavyofaa
Kabla hujajumuika humu ulikuwa hujifunzi huko kwingine na kwanini hujaendelea kuwa tu msomaji hadi uwe member?
 
Kabla hujajumuika humu ulikuwa hujifunzi huko kwingine na kwanini hujaendelea kuwa tu msomaji hadi uwe member?
Okay, nimeamua kujisajili kama member ili nipate kibali cha kushiriki mijadala inayokuwa inaendelea humu kitu ambacho mwanzoni sikuweza nilipokuwa napita kama msomaji/mgeni.
 
Mbona umeenda mbali hivyo kiongozi, kusema mna roho nzuri ilikuwa ni imani yangu kwenu na mpaka sasa imeshajidhihirisha ndiyo maana mmeitikia wito wangu wa kuwaomba mnipokee hivyo sioni kama kuna ubaya wowote hapo.
Kama wewe siyo mtu mbaya tunayemdhania nisamehe Mkuu.
Juzi kuna mtu kaja na thread hapa JF ya kuomba msaada wa kifedha akamtibie mwanaye, kwa "roho nzuri" unayoisema wewe akasaidiwa. Baada ya kusaidiwa, waliyomsaidia wakagutuka ya kuwa wametapeliwa.
Kwahiyo ulivyokuja na ID mpya kwa kauli ya "wana JF mna roho nzuri" tukajua huenda ni yule member tapeli aliyetapeli watu kaja kutudhihaki kwa shukrani ya "ahsanteni wanaJF kwa roho zenu nzuri"
Karibu JF.
 
Ni mara yangu ya kwanza kujiunga na JF wala sina wasi wasi yoyote najua wanajukwaa ni watu wastaarabu na wakarimu hivyo mtanionyesha ushirikiano wa hali na mali.

Sina mengi ya kusema ila naamini kwa hayo machache mtanipokea na kunitambua kama mwanajukwaa mwenzenu. Je wangapi mko tayari kunipokea mimi kama mwana JF mwenzenu?? Ningependa kusikia mrejesho wenu juu ya ombi langu.
Ila siku hazifanani
 
Back
Top Bottom