Nazjaz, unataka kumfanyia mwanao majaribio????
Kama unataka uwe sampo, anza kukaa mlangoni hadi siku ya kujifungua ndio utajua wahenga wana la maana ama lah.
Wazungu kukosa evidence haimaanishi kitu hakipo.
Kwa maelezo zaidi nenda jukwaa la dokta hii mada imejadiliwa kwa kirefu.
Natumia mchina siwezi weka link hapa.
Dada yangu angalia hao wapita njia wasikudanganye ukaingia mahali ambapo sio. Mwisho watakwambia ukifikia wakati wa kujifungua nenda kwa mganga wa kienyeji ukajifungulie huko. Peleka IMANI yako kwa Mungu.
uliyenaye anakataa kutoka ng'o.
Utaingia sieta hiv hiv.
mh, hivi huwa yana ukweli haya?
jifanyie majaribio, utapata jibu zuri bila changa.
Sangari wanawake wengi wanakuwa na hofu sana wakikaribia kujifungua, hasa mtoto wa kwanza.
Tatizo ni kwamba wakati nchi nyingine uzazi ni neema, huku kwetu uzazi ni nusu ya kifo