Kama nitakuwa nimekosea utaniwia radhi mkuu, umesema umepata kazi katika chuo kikuu kimoja kama T.A, lakini wakati huo huo unasubiri kazi ya Ualimu toka serikalini, napata wakati mgumu kidogo kutokana na maelezo yako kwa sababu moja kuu, serikali huwa haiwapangii kazi walimu kwenda kufundisha vyuo vikuu labda kama utaratibu umebadilika ama ni kutokujua kwangu ila nijuacho mimi serikali huwapanga walimu wa sekondari na sitaki kuamini kwamba Ajira ya serikali unayoisubiri ni kwenda kufundisha A-Level.
Other things remain constant, ulicho nacho mkononi ndio chako.................. nenda kafanye kazi zikitoka hizo za serikalini utaangalia ulikopangiwa na mkataba wa hapo ulipo ukoje then itakuwa rahisi kufanya maamuzi.