Pole sana kaka. Kupenda ni ugonjwa MBAYA SANA! Unaona kabisa kuwa anakuelekeza kuzimu, lakini bado unamtaka. Kwa namna hiyo hata wa ku cover nafasi yake si rahisi umwone.
Kama ni kwekli anakupenda kama unavyompenda, asingerudia kosa. Pili jaribu kumdodosa kwa upole, ni nini anachokosa kutoka kwako, mpaka akusaliti. Ukikijua angalia kama unaweza kukirekebisha. Kama huwezi, jua umepotea, achana naye, hutakufa kwa kumkosa yeye. Je, angekufa leo(siombi afe) natoa mfano tu, ina maana wewe usingeishi????
Tatu, wewe una mke, hakuna baraka za Mwenyezi Mungu ktk uhusiano wenu. Bora umwombe Mungu akusamehe, kisha akupe nguvu za kumshinda Ibilisi. Utulie ndani ya ndoa yako. Je, mkeo angefanya kama unavyofanya wewe, ungejisikiaje? Usimtendee usichopenda kutendewa.
Math 7:12.
MWISHO: Huyo hawara anajua kuwa hana future na wewe, sababu ana mke. Kwa hiyo sana sana akuchune tu, na mchezo mchafu huo. HAKUNA MAPENZI YA DHATI HAPO. Toka kwenye utumwa wa mapenzi.