Wana Simba Nina zawadi yenu ya wimbo huu mpya

Prince05

Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
43
Reaction score
84
Wimbo huu nimeufanya kwa kushiriaka na AI, nilipata wazo, nikatunga mashairi machache. Nilipopata ugumu nikashauriana na AI tukajadili tukapata mashairi.

Nikafanya prodction ya Beat kama sample, nikashirikisha AI kuboresha zaidi kwa maelekezo yangu nini nataka kiweje, nataka sound zipi nk. Tukafanya sauti, mixing, mastering wimbo ukatoka. Hii sehem fupi ya wimbo wa SISI NI SIMBA.
Your browser is not able to display this video.
 
Ruge aliwahi kupasua CD ya Nandi bila hata kudikiliza wimbo hata mmoja akamwambia Nenda kaboreshe zaidi Kazi Bado sana.

Na mimi sijasikiliza lakini Nenda kaboreshe zaidi na zaidi, Kazi bado sana.
 
Wimbo ni mzuri,ila sijajua kama umefika mwisho.
Kama hapo ndio mwisho basi utakua umefanya vizuri.
Maana sijasikia jina hata moja la mchezaji au kiongozi wa Simba.
Kosa wanalofanya au walilofanya watunzi wengi wa nyimbo za Simba na Yanga ni kutaka majina ya wachezaji na au Viongozi,kosa la kutakaajina ni pale hao wachezaji au Viongozi siku wakiondoka katika timu hizo wimbo huo utakua umepoteza kabisa maana.
Mfano mzuri wa wimbo mzuri ni ule unaoimba Simba bila kutaja majina ya watu.wimbo wa Ali kiba.
Sasa na wimbo wako ni unafaa kwa sababu hautaji majina ya watu,hivyo utaishi muda mrefu ukiwa bado una maana.
Ila kama hauna lengo la wimbo kuishi muda mrefu unaweza kuweka majina.
Hongera sana.
 
Hongera mkuu....
Kumbe AI inaweza mambo mengiii
 
Nyimbo nzuri, boresha mashairi yalete vibe ili nyimbo iishi. Ili nyimbo iwe ya mashabiki ifanye iwe rahisi kuiimba, pasiwe na note za juu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…