Uchaguzi 2020 Wana-Ubungo tupewe nini tena? Kitila Mkumbo ni bahati ya mtende

Uchaguzi 2020 Wana-Ubungo tupewe nini tena? Kitila Mkumbo ni bahati ya mtende

Minaely mimi

New Member
Joined
Aug 29, 2020
Posts
2
Reaction score
2
Imezoeleka kuwa Jambo juzi na jema kutokea kwenye jamii au maisha ya mtu,tunaiita BAHATI ya MTENDE.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa wakazi wa jimbo la ubungo na halmashauri ya ubungo.

Chama Cha mapinduzi chini ya mwenyekiti wake,jembe,chuma mpambanaji ,Rais John Pombe Joseph Magufuli kimetupa kijana mahiri kwa ujengaji hoja,mtu makini kwa usimamizi wa rasilimali za umma,na mtu mwenye moyo wa upendo,kujitoa na uzalendo kwa nchi yake.Anaitwa Profesa Kitila Mkumbo kuwa mgombea wa ubunge.

Nasema Kitila Mkumbo ni bahati ya MTENDE kwa Wana ubungo kwasababu.

1 : Kitila ni mwenyeji wa jimbo hili kwa zaidi ya miaka ishirini na tano.maisha take yote ya upambanaji ameyafanya akiwa ni mkazi wa ubungo na hata siku moja hatujawahi kusikia akihusishwa na matendo machafu,yakihuni yenye kuharibu sifa yake,Watanzania wenzake wala mji wetu.

2: Ni mbobezi wa tafiti zinazohusu kero na mahitaji ya jamii..hivyo anayajua vyema matatizo na mahitaji ya jamii

3: Ni mtu mwenye kutoa suluhisho za kero za jamii kuliko malalamiko ( refer ilani ya Chadema 2010,ya ccm 2020) na hata tafiti zake mbalimbali akiwa chuo kikuu

4: Ni mchapakazi asiye penda makuu ila kutimiza wajibu na uhitaji wa jamii (pitia kazi zake tangu amekua katibu wa wizara ya maji)

5: Anajua kuishi na watu ,na mnyenyekevu kwa watu...hii ndio sababu kubwa inayomfanya kupendwa Sana kila alipofanya kazi (chuo kikuu UDSM,CHADEMA,ACT WAZALENDO NA SASA CCM & SERIKALI KUU )

Mwisho kabisa Profesa Kitila Mkumbo ni mtu wa kuheshimu mawazo na ahadi zake.na ahadi yake kuu kwa wananchi wa ubungo anasema
"NOAMBA KAZI KWA WANANCHI,NYIE NDIO MABOSI ZANGU,NITAKUA MTII NA MNYENYEKEVU KWENU,NA NITAPATIKANA MUDA WOTE KWENU ILI NIWEZE KUWATUMIKIA"
 
Anapita huyo kwa kura nyingi.Ni mmoja kati ya wabunge wanaotarajiwa kuunda cabinet possibly he gonna hold ministry of water. Think takers wa CCM
 
Kikubwa ni kwamba kila mwana ccm atabeba mema au mabaya ya Jpm. Hataangaliwa kama yeye si aliunga mkono juhudi!
 
Pumbafu zako, kwani Mkumbo amekupa shs ngapi uje utoe uharo wako hapa
Mkuu umekosea, hata wewe unaweza kuleta yule anayeona anafaa zaidi na ukaweka hoja zako,kipindi hiki kila mtu anauhuru...... Tutumie lugha za staha tu
 
Mkumbo ndio yule jamaa akiongea anatoa povu mdomoni.
Nilimuona juzi ITV sikujua kama ndio yeye,maana nikaona anaongea pumba tupu.
 
..Prof.Kitila Mkumbo amelifanyia nini jimbo la Ubungo tangu awe katibu mkuu wizara ya maji?
 
Ccm Hamna kitu cha ajabu mtachofanya kwenye hii nchi labda mbadili hiyo katiba yenu mliyojitungia kwanza.
 
Kitila sio Mwana Ubungo kabisa alikimbia Iramba ambako aliwekeza miaka yote kwa nini !? Huyu ni pandikizi na hatufai. Ameshindwa kujibu kuhusu nyumba za watu kuvunjwa kinyume na sheria ikiwa kulikua na zuio la mahakama.

Wana Ubungo mtafanya kosa kubwa kumchagua huyu Kitila. Afadhali kukaa bila mbunge kuliko Mbunge wa kambo.
 
Back
Top Bottom