A Peculiar people
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 612
- 773
Kama ni hivi balaa...MATOKEO YA UCHAGUZI WA TFF:
RAIS
1. Wailes Karia 95( simba)
MAKAMU WA RAIS
1. Marco Wambura 85(simba)
WAJUMBE WA KANDA
1 Salum Chama (simba)
2 Vedasto Lufano (simba)
3 Mbasha Matutu (simba)
4 Sarah Chalo (simba)
5 Issa Bukuku (simba)
6 Kenneth Pesambili (simba)
7 Elias Mwanjala (simba)
8 James Mhagama (simba)
9 Dastan Nkundi (simba)
10 Mohamed Abeil ( simba)
11 Francis Ndulane (simba)
12 Kharid Mohamed (simba)
13 Lameck Nyambaya (simba)
Hii ni bahati mbaya, mpango, au...
Baada ya kushindwa uwanjani na kusajili shikamoo jazz..... Wakaona ni bora kutengeneza mazingira ya point za mezani
Simba tunataka fear tu. ....hatutaki kubebwa. ....japo maamuzi yakiwa fear yanga wataona kama wanaonewa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umeliona baada ya madega kupigwa chini?Ndo maana soka letu haliendelei..
Manji kachangia Nn sasa wakati malinzi ndo aloibeba yangaHoja zako kama za Bi Hindu na akina Mzee Akilimali, kwahiyo hujui mchango wa Manji kwa hiyo miaka 4?
Umemsahau Bi. Hindu ni Simba toka enzi ya SunderlandHakuna furaha ambayo mwana Simba SC yoyote anayo leo ukiachia mbali ile ya kuwa na Kikosi cha Mauaji ya Shalubela baada ya kufanya Usajili wa Kufa Mtu na ushindi murua kabisa wa leo wa Wanasimba wenzetu wa kutupwa kama siyo wa kugalagaza na kindakindaki Rais mpya wa TFF Wallace Karia na Makamu wake Michael Wambura.
Nakumbuka kabisa miaka minne iliyopita Wanasimba tuliteseka na kunyanyasika mno baada ya aliyekuwa Rais wa TFF Jamal E. Malinzi kusikika kila mara akisema tena kwa dharau na kutamba kabisa kuwa ndani ya Uongozi wake wa miaka minne ( 4 ) Klabu ya Simba isahau Ubingwa wa VPL na kwamba Yanga FC ndiyo itakuwa Bingwa kwa gharama zozote / yoyote na kweli ilikuwa hivyo japo kwa mwaka wake wa Kwanza Azam ilichukua Ubingwa.
Kama tunavyojua kuwa Mwenyezi Mungu siku zote huwa hamtupi mja wake na hatimaye leo huko Mkoani Dodoma katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF ) pamoja na Malinzi kupeleka taarifa zake kichinichini kwa Wajumbe huku akiwataka wamchague kati ya Madega na Mayai ili ule Uyanga ndani ya TFF uendelee haikuwa hivyo ambapo kwa msaada mkubwa mno wa Malaika wa Mungu waliopita ni wana Simba SC watupu tena ambao ni Wanachama hai kabisa Wallace Karia na Michael Wambura.
Na ndiyo maana hata baada tu ushindi ule akina Madega, Mayai, Mwakalebela na wana Yanga waliokuwepo pale Ukumbi wa Mtakatifu Gasper walipigwa na butwaa sana huku wakiwa wamenywea kabisa na kuanza kukaa katika Vikundi Vikundi wakilaumiana kwamba kwanini Mikakati yao imeshindikana huku wengine wakisikika wakisema kuwa na Wao Yanga FC sasa hii miaka minne ( 4 ) ya akina Karia na Wambura ni ya kuwa tu Wavumilivu kwani lazima tu na Simba nao watalipiza Visasi walivyokuwa wakifanyiwa na Malinzi.
Yaani hadi raha kwani unaambiwa........
- Baba Magufuli ni Simba SC
- Mama Samia ni Simba SC
- Kaka Majaliwa ni Simba SC
- Spika wa Bunge la JMT Job Ndugai ni Simba SC
- Waziri wa Michezo Mwakyembe ni Simba SC
- Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo hata TFF ilipo Paul Makonda ni Simba SC
- 80% ya Wajumbe wapya wa TFF waliochaguliwa leo ni Simba SC
- Mwenye dunia yake na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana ni Simba SC
- Malaika wote wa Mbinguni ni Simba SC
- GENTAMYCINE mwenyewe ni Simba SC
- 98% ya JamiiForums Members ni Simba SC
- Makomandoo wetu Tanzania wote ni Simba SC
- 75% ya Watanzania wote ni Simba SC
- 95% ya Matajiri wote nchini Tanzania ni Simba SC
- 99.9% ya Wanawake warembo wote nchini Tanzania ni Simba SC
- 100% ya Wasomi wote nchini Tanzania ni Simba SC
- Wanajeshi wote wanaofanya Mazoezi ya pamoja Tanga ni Simba SC
- Wanaume wote wenye nguvu za Kiume na Wanawake wasio Wagumba ni Simba SC
- 99% ya Wanafunzi wenye akili Shuleni na Vyuo Vikuu ni Simba SC
Yaani kuna Watu miaka hii minne ( 4 ) ya akina Karia na Wambura watapigwa goli saba ( 7 ) tu kila tutakapokuwa tunakuana nao na kama haitoshi na Sisi Simba SC sasa tunataka tuweke rekodi ya Kuuchukua Ubingwa wa VPL kwa miaka yote hii minne ( 4 ) ambayo wana Simba SC wenzetu akina Wallace Karia na Michael Wambura watakuwepo Madarakani.
Tutaheshimiana tu Mungu mkubwa!!!!!!!
Kwahiyo akifa Manji yanga inakufa? Alikuwepo Gulamali nadhani ulikuwa bado hujaiona dunia enzi hizo au unamkumbuka Babu Viran?Hoja zako kama za Bi Hindu na akina Mzee Akilimali, kwahiyo hujui mchango wa Manji kwa hiyo miaka 4?
Umesema kweli kabisa , kama watu wao waligombea ili kuipa Simba ubingwa watasubiri sana.Waulize kama kikwazo kilikuwa ni Malinzi, kwa nini wakawa wanasajili timu mpya kila mwaka? Hao wachezaji walikuwa wakisajiliwa kupambana na Malinzi, au ni kwa sababu waliowatangulia walikuwa wabovu? Na huo usajili mbovu uliosababisha hayo ulifanywa na Malinzi? Kiongera, Serunkuma, Diop Na kama hao, walilazmishwa na Malinzi kuwasajili? Malinzi ndiye aliyewalazimisha waamuze Tambwe aliye kuja kuibeba Yanga? Malinzi ndiye aliyewalazimisha kubadili makocha kama shati ndani ya kipindi hicho? Wasipotafuta sababu ya kweli ya miaka minne hiyo, wanaweza kuendelea na minne mingine. Kikosi cha kufa mtu tu siyo kinacholeta ushindi. Mshairi mmoja alipata kusema 'Stone walls do not a prison make, nor iron bars a cage'. Yaani kuta za mawe sizo zinazofanya gereza, wala kizimba (hakijengwi) kwa fito za chuma (pekee).'
Kama kweli hao waliotajwa kuongoza TFF wote ni wanachama/wapenzi wa Simba, na kama kweli huo ulkuwa ni mkakati mahsusi wa Simba, basi wategemee anguko endelevu takatifu. Kwa nini? Mzazi ambaye ni mwalimu wa mwanafunzi wake mwenyewe darasani, anayemwonyesha maswala a mtihani na kumpa majibu yake ili afaulu, huishia kumgeuza mwanafunzi huyo kuwa kihiyo, huku wenzake wanaohngaika kwa uwezo na nguvu zao wakiendelea kuelimika inavyostahili hata kama hawabebi nafasi ya kwanza darasani. Wanapoingia darasa au shule nyengine ambayo mwalimu-baba hana mamlaka nayo, wanafunzi wa aina hiyo hugeuka ghafla kutoka wa mfano kuwa ni kituko.Umesema kweli kabisa , kama watu wao waligombea ili kuipa Simba ubingwa watasubiri sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Fear!!!!Simba tunataka fear tu. ....hatutaki kubebwa. ....japo maamuzi yakiwa fear yanga wataona kama wanaonewa.
Sent using Jamii Forums mobile app