Wana Yanga SC mlisema kuwa Haji Manara hakumtukana Rais Karia je, baada ya Kumuomba Radhi na Kukiri Kosa mnajionaje?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwa nasema Mashabiki wa Yanga SC mna Matatizo mengi Ubongoni mwenu msiwe mnakasirika.

Mlisema Haji Manara hakutukana na wala hakutenda Kosa na mkapa Kiburi kuwa mtamtafutia Malori Saba ya Wanasheria wakamtetee hatimaye Mwenyewe amekiri Kosa na hata Kujutia pia.

Kuna Siku hapa hapa JamiiForums GENTAMYCINE niliandika Uzi kuwa Yanga SC wawe Makini sana na Haji Manara na jinsi wanavyomdekeza na kumpa Uhuru usio na Mipaka kuwa kuna Siku atakuja Kuigharimu na Kuiponza Klabu yenu hamkunielewa ila taratibu sasa nadhani Utabiri na Maono yangu yanakaribia.

Halafu alivyo Mental anasema ( Haji Manara ) kuwa hakumtukana Rais wa TFF Wallace Karia. Sasa kama hakumkosea na wala hakumtukana huo ( huu ) Msamaha aliomuomba ni wa nini?

Yanga SC endeleeni tu Kumlea HM.
 
Ni wapi kwenye maelezo ya Manara kakiri kutoa matusi? Ameomba radhi kwa kujibizana. Rudi shule ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…