Wana Yanga SC wenzangu nashauri Kikosi chetu cha Kumuua Mnyama Jumamosi kiwe hiki

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
  1. Ben Kakolanyi
  2. Ramazan Kessy
  3. Haji Mwinyi
  4. Patrick ( Pato ) Ngonyani
  5. Nadir Haroub ( Nahodha )
  6. Juma Makapu
  7. Geofrey Mwashiuya
  8. Raphael Daud
  9. Emanuel Martin
  10. Donald Ngoma
  11. Amis Tambwe
Nina uhakika kabisa wana Yanga SC wenzangu hasa tuliopo humu Jamvini JF mtakubaliana kabisa na Mimi Mwana Yanga mwenzenu wa ' Kutukuka ' kabisa GENTAMYCINE kwamba ama hakika kwa Kikosi hiki Mnyama ( Simba SC ) hatoki siku hiyo na tukimkosa kosa sana basi kwa Kikosi hiki tu tunamfunga Goli 5 au 7.

Kwakuwa GENTAMYCINE nipo karibu sana na Kocha wetu George Lwandamina na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa naombeni maoni yenu ya haraka haraka ili kama Kikosi hiki mmekiridhia basi nikamkabidhi haraka Kocha ili nae ' akibariki ' na kipelekwe upesi kwa ' Mganga ' wetu kule ' Matombo ' na ' Mang'ula ' Mkoani Morogoro ili wakapikwe vyema Kindumba / Kiuchawi kusudi Simba SC afungwe Jumamosi Shamba la Bibi.

Nawasilisha.
 
sijamwona tshishimbi papa kabanga, ajib
 
Unajitekenya mwenyewe halafu unacheka.
 
Kwenye list yako ni wawili wanaweza kuanza.
Imefika mahali wa Msimbazi anapanga Kikosi cha Jangwani.
Kipigo kipo pale pale. Yanga ataingia kama underdog dhidi ya Kikosi cha 1.3 billion.
Nyingi katika hizo 1.3 billion ziliishia kwa Makofia, Aveva na Kaburu, watoto wa mjini.
 
nasubiri utabiri wako mkuu,maana wewe ni bingwa wa utabiri kama Pweza Paul
 
Mara Simba mara Yanga siku ingine Mtz siku ingine mnyarwanda. Mradi upate cha kupost tu siku isogee.
 
Mara Simba mara Yanga siku ingine Mtz siku ingine mnyarwanda. Mradi upate cha kupost tu siku isogee.

Inaonekana uwepo wangu humu ' unakukwaza ' na ' unaumia ' sana Mkuu. Kwani Mimi kuwepo humu ndiyo nakusababishia hayo maisha yako magumu na ya ' Kimasikini ' kuzidi kukuandama? Hapa najinunulia internet bundle mwenyewe unanichukia hivi ingekuwaje kama Wewe ndiyo ungekuwa unanipa hela ya bundle? Pumbavu Wahed Wewe pambana na hali yako na acha kupoteza muda wako na ' Purely Talented and Charismatic Felle ' GENTAMYCINE kwani hutoniweza na unaweza hata ukajikuta unakuwa taahira / chizi kwa ' Kunichukia ' Mimi huku mwenzako maisha yangu yakiwa katika ' mteremko ' halafu natiriririka na naserereka nayo kwa raha zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…