Wana Yanga SC wenzangu tusikubali huu usajili wa kiini macho tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwa kama Mwanachama ' lia lia ' wa Yanga FC natoa masikitiko yangu makubwa kwa Uongozi wa Klabu yetu hasa kwa aina hii ya usajili ambao wanaufanya kwani kiukweli kuna Wachezaji ambao Mimi binafsi sioni kama wanastahili kuendelea kuichezea Yanga.

Kila Mtu anajua kuwa Wachezaji kama Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ni ' wabovu ' na ' wamechoka ' sana kiasi kwamba hawatakuwa na faida tena kwa Klabu yetu hasa huko tuendako na yawezekana tukaja kujuta pia.

Kosa lingine kubwa ambalo nina uhakika wa 100% kwamba litatugharimu ni kitendo kibaya na cha kusikitisha cha Uongozi wetu wakiongozwa na Makamu Rais Sanga na Katibu Mkuu Mkwasa bila kusahau ' Kamati ' nzima ya ' Usajili ' kwa kumsajili mchezaji ambaye ni ' mbovu ' na hata huko alikotoka alikuwa anaanzia ' benchi ' aitwa Ibrahim Ajib.

Sasa kituko kingine ambacho ndiyo kinanipandisha hasira Mimi mwana Yanga FC ni hiki kitendo cha kutaka kumsajili Mchezaji ambaye kiukweli hajui kabisa mpira kutoka nchini Congo aitwae Tshimbimbi. Nimemjua huyu Mchezaji siku nyingi na kumfuatilia na sijaona uwezo wake wowote hivyo naona ni bora tu hata Justine Zulu ' mkata umeme ' akabaki tu.

Jamani wana Yanga FC wenzangu hebu tusibaki nyuma katika hili kwani tunafanya ' Usajili ' mbaya na mbovu ambao haujawahi kutokea katika historia ya Timu na kama tusipokuwa makini kuna uwezekano mechi yetu na ' Watani ' zetu Simba SC tarehe 23, August 2017 tukatafuta mahala ambapo tutaficha ' Sura ' zetu kwa aibu ya Kipigo kitakatifu na cha Shalubela.

Yanga FC daima
Yanga mbele kwa mbele
Yanga ya Kimataifa

Kama Wewe ni mwana Yanga FC mwenzangu tafadhali upatapo tu uzi huu hebu mfowadie mwana Yanga mwenzako na kwa aliye karibu na Viongozi wa Yanga akina Sanga na Mkwasa bila kuisahau ile Kamati nzima ya Usajili basi ' wafowadieni ' pia na huu uzi ili uwafikie haraka na ushauri wangu huu wa ' Kutukuka ' uweze kuzingatiwa na kufanyiwa Kazi kwa manufaa ya Klabu / Timu yetu.

Kila la kheri.
 
Wachezaji wazuri ndio wakaoje tuabarishe mkuu
 
Umetumia mda wako mwingi sana kuandika ujinga yote haya kasababisha mh rais magufuli Kubana ajira kwa vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…