Wana Yanga SC wenzangu tusikubali huu usajili wa kiini macho tafadhali

Bahati Mbaya umetoa tu mapovu ila haujatoa nini suluhisho

Udaku huu peleka huko mikia a.k.a mezani fc Tuachieni yanga yetu
 
Jitahidi unywe sumu maana hakuna namna nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa kama Mwanachama ' lia lia ' wa Yanga FC natoa masikitiko yangu makubwa kwa Uongozi wa Klabu yetu hasa kwa aina hii ya usajili ambao wanaufanya kwani kiukweli kuna Wachezaji ambao Mimi binafsi sioni kama wanastahili kuendelea kuichezea Yanga.
Ukiwa 'kama' mwanachama; kumbe siyo mwanachama.

Huna lolote Mkuu.
 
Kichwa kikubwa kwa ajili ya kutenganisha maskio tu....

KIMEO CHANGU
 
Basi tufanye hivi...

Weka idadi ya misimu aliyocheza Bongo akiwa na simba SC , na amrisaidia timu yake kubeba VPL mara ngapi katika hiyo misimu?[emoji23]

Aliisaidia Simba kwa jambo hili

 
Aliisaidia Simba kwa jambo hili

View attachment 552473
Hakuwa na msaada wowote. Kipindi hicho klabu ilikuwa katika mgogoro mzito wa uongozi na Mwenyekiti (Lloyd Nchunga) aligoma kujiuzulu hivyo hiyo mechi ilitumika kumng'oa madarakani. Kati ya magoli matano; matatu yalikuwa matuta, wewe huwezi kujiuliza kulikuwa na nini?
 
KABLA hata msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na majukumu yake haujaanza, nadhani ipo haja kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kumwelewa na kumfahamu mapema mkuu wao mpya wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Dismas Ten.

Ten ameajiriwa na Yanga hivi karibuni akitokea klabu ya Mbeya City ambako nako alikuwa kwenye nafasi kama hiyo.

Kwa nini wana Yanga wanapaswa kumfahamu mapema Dismas Ten? Jibu ni rahisi tu kuwa kuna mabadiliko fulani ambayo idara yake ya habari na mawasiliano ndani ya Yanga itakumbana nayo tofauti na maisha yaliyozoeleka hapo awali.

Badiliko la kwanza la kawaida ambalo Yanga watarajie kuliona chini ya usimamizi wa Ten, ni idara yao ya habari kuweza kuimarika zaidi katika upashaji wa habari mbalimbali za masuala yote yanayoihusu klabu hiyo.

Hatubezi mfumo wa upashaji habari ambao Yanga walikuwa nao hapo nyuma kabla ya ujio wa Ten, lakini ulikuwa na udhaifu fulani ambao yeye na msaidizi wake Godlisten Anderson bila shaka wameshaanza kuutafutia dawa.

Hapo kabla Yanga ilikuwa ikitumia kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti kufikisha habari kwa mashabiki wake na wadau wa soka nchini huku ikiachwa nyuma katika upashaji habari kwa kutumia mitandao ya kijamii kama Twitter, Instagram na Facebook.

Hata tovuti ya Yanga nayo ilikuwa kama mfu, jambo lililonyima kundi kubwa la wanachama na mashabiki kupata habari zinazoihusu klabu yao. Hii iliwaathiri pia hata wadau wengine wa soka kuzijua habari za Yanga.

Haikuwa sahihi kwa Yanga inayotajwa kama klabu inayoongoza kwa idadi kubwa ya mashabiki hapa nchini, kushindwa kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia tofauti na Simba, Azam, Mbeya City na Mtibwa Sugar ambazo zimekuwa mfano wa kuigwa katika upande huo.

Kwa dunia ya sasa, mitandao ya kijamii na tovuti pekee vinaweza kuwa chanzo imara cha mapato kupitia matangazo yatakayowekwa huko, lakini pia inavutia wadhamini kuweka fedha zao kwenye klabu wakiamini kuwa taarifa za huduma zao zitafikia walengwa kirahisi na kwa haraka.

Kwa hapa nchini, mfano wa klabu iliyonufaika na hili ni Mbeya City ambayo tovuti yake imesaidia kuvutia kampuni kama Sports Masters, Binslum Tyres, Bhojani Chemists na Coca Cola kuidhamini. Kwa wasiofahamu tu ni kuwa Dismas Ten ndiye ambaye aliianzisha na kuifikisha tovuti ya Mbeya City hapo ilipo.

Lakini pia jambo lingine ambalo bila shaka tulitegemee kuliona kwa Ten ni kwenda kinyume na utamaduni uliozoeleka na mashabiki katika namna ya kuwasilisha habari za klabu hiyo uzingatiaji mkubwa wa weledi katika utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga.

Kama walizoea matumizi ya lugha za matusi, mipasho na kejeli sidhani kama watazisikia au kuzisoma katika mazungumzo au maandishi yake. Huyu ni mtu anayejiheshimu na kuheshimu taaluma na wajibu wake tofauti na kundi kubwa la maofisa habari wa klabu zetu ambao wamekuwa hawazingatii weledi katika majukumu yao.

Kwa bahati mbaya, Idara ya Habari katika soka letu haipewi heshima stahiki na imekuwa ikidharaulika kuanzia katika Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) hadi kwenye klabu zetu, tofauti na nchi nyingine ambapo inapewa uzito mkubwa na kuheshimiwa.

Hii inatokana kwanza na utashi finyu wa viongozi katika kutambua umuhimu wa idara hiyo, lakini pia hata wasimamizi wa idara hizo nao wameshindwa kuwa na mikakati imara ya kuhakikisha kitengo cha habari kinapata thamani stahiki.

Wakati umefika sasa kwa klabu na mamlaka zinazosimamia soka kubadili mitazamo na hisia potofu za kuitazama Idara ya Habari kama kitengo cha ziada tu na kipo kwa ajili ya kuzungumza na vyombo vya habari kama ilivyozoeleka.

Badala yake idara hii inatakiwa ipate watu sahihi watakaofanya mambo kwa weledi na ubunifu wa hali ya juu, ili iwe chachu ya kuleta maendeleo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

Kwa muda mrefu takwimu na taarifa muhimu zinazohusu wachezaji wa Yanga na timu kwa jumla, zimekuwa adimu licha ya timu hiyo kuwa na Idara ya Habari ambayo ndio yenye jukumu la kushughulikia masuala hayo.

Pengine uongozi wa Yanga umegundua udhaifu huo na kuamua kumchukua Ten ambaye anaonekana ni tiba sahihi wa changamoto zinazoikabili Idara ya Habari ya Yanga.

Hata hivyo, watu wa Yanga wanatakiwa kumvumilia tu Dismas Ten kwani atayatimiza majukumu yake kwa ufasaha pasipo kupiga kelele au kutoa lugha za kejeli na mipasho kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kama ilivyokuwa imezoeleka siku za nyuma , pamoja na kwamba mambo hayo yanapendwa sana na mashabiki wengi wa soka hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…