kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Kama kuna watu wanakosa raha kwasababu ya timu hii
Mimi wa kwanza, hii timu kila wanapofanya vibaya hakika mimi nakosa raha sana na tena mazingira yangu, familia yangu yaani wazazi na ndugu zangu wote ni Simba, wakifanya vizuri tu nyumbani hapakaliki.
Na vurugo, nachekwa mpaka nakosa raha. Msimu huu nilitamba ni lazima Yanga tufike robo fainali maana tuna wachezaji wazuri wenye uwezo na kila kitu, ila maskini ya Mungu safari yetu ya kusonga mbele naona kama imefika mwisho.
Ila nilitafakari sana juu ya timu hii, nilichokuja kugundua ni kwamba sisi Yanga siyo kwamba hatuna uwezo wa kufika makundi au sio kwamba hatuna timu nzuri, bali tunachokikosa ni bahati tu. Unajua bahati ndiyo kila kitu.
Ila nikajiuliza nini tufanye ili tuwe na bahati kama wenzetu? Nikaja kundua kuwa sisi mashabiki ndiyo tuna ufunguo wa timu yetu. Nina maana gani kusema hivi? Yaani sisi mashabiki tupige dua kiombea timu yetu na nina amini tutatoboa tu.
Nini tufanye ili kuombea timu yetu? Ni lazima kila mwana Yanga siyo wote, wale ambao wanapenda timu yao, tuchukuwe karatasi na kalamu, andikeni majina ya wachezaji wetu wote halafu ukisha maliza, halafu upande mwingine una andika maneno haya;
"Hoba Hoba Hoba Hoba hiba, kwa uwezo wako ee Mwenyezi tusaidie, hatuna msaada mwingine zaidi yako. Japo tuna jichanganya na mambo mengine lakini bado tunajua kwako ndiyo kuna msaada tosha wa kusaidia timu yangu (Yanga)"
Chukuwa karatasi hiyo na udogo wa chini yani wa Tanzania, weka ndani ya karatasi alafu funga na kamba. Unaweza fungo ilo chini ya kitanda chako alafu tukutane Jumapili tuone kitakacho tokea.