Wana Yanga wenzengu tutumie sherehe hii kuiombea Yanga

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kama kuna watu wanakosa raha kwasababu ya timu hii
Mimi wa kwanza, hii timu kila wanapofanya vibaya hakika mimi nakosa raha sana na tena mazingira yangu, familia yangu yaani wazazi na ndugu zangu wote ni Simba, wakifanya vizuri tu nyumbani hapakaliki.

Na vurugo, nachekwa mpaka nakosa raha. Msimu huu nilitamba ni lazima Yanga tufike robo fainali maana tuna wachezaji wazuri wenye uwezo na kila kitu, ila maskini ya Mungu safari yetu ya kusonga mbele naona kama imefika mwisho.

Ila nilitafakari sana juu ya timu hii, nilichokuja kugundua ni kwamba sisi Yanga siyo kwamba hatuna uwezo wa kufika makundi au sio kwamba hatuna timu nzuri, bali tunachokikosa ni bahati tu. Unajua bahati ndiyo kila kitu.

Ila nikajiuliza nini tufanye ili tuwe na bahati kama wenzetu? Nikaja kundua kuwa sisi mashabiki ndiyo tuna ufunguo wa timu yetu. Nina maana gani kusema hivi? Yaani sisi mashabiki tupige dua kiombea timu yetu na nina amini tutatoboa tu.

Nini tufanye ili kuombea timu yetu? Ni lazima kila mwana Yanga siyo wote, wale ambao wanapenda timu yao, tuchukuwe karatasi na kalamu, andikeni majina ya wachezaji wetu wote halafu ukisha maliza, halafu upande mwingine una andika maneno haya;

"Hoba Hoba Hoba Hoba hiba, kwa uwezo wako ee Mwenyezi tusaidie, hatuna msaada mwingine zaidi yako. Japo tuna jichanganya na mambo mengine lakini bado tunajua kwako ndiyo kuna msaada tosha wa kusaidia timu yangu (Yanga)"

Chukuwa karatasi hiyo na udogo wa chini yani wa Tanzania, weka ndani ya karatasi alafu funga na kamba. Unaweza fungo ilo chini ya kitanda chako alafu tukutane Jumapili tuone kitakacho tokea.
 
Wachezaji muwapeleke kwa mwamposa wale keki na mafuta ndio wawe wanaondoka.

Yanga ovyo sana.
 
Team Haina Uwezo Wewe Unahangaika Nayo! Ya Nini Sasa Iache Yenyewe
 
Oooh jamani ila kwakweli nikiri wazi ww ni mshabiki uliejitoa kwa hari kubwa kuitetea Yanga kuwa itafuzu nachokwambia kwa sasa usikate tamaa maana karibia mgonjwa ataingizwa theater kwa upasuaji hivyo muombee atoke hai. Mengine ni majaaaaliwa
 
MIAKA 23 TOKA NYERERE AFARIKI UTOPOLO HAIJAWAHI KUFIKA MAKUNDI CAF[emoji17][emoji17][emoji17][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji2357][emoji2357][emoji2357][emoji2357][emoji2357]
 
Daah..huu c ushabik tena ila ni ukichaa...yaan uache kusajili wachezaji wazur eti kisa kujq kutegemea miujiza ya Mungu ili uvuke grp stage..ingekuwa hivo akuna timu ligi ya NBC wangesajili..ni mwendo wa kwenda kwa Mwamposa tu na timu inafanya vzur...tatizo lq yanga huwa viongoz hawatak kusema ukwl kwq mashabik....wameishia kuwalipa waandish uchwara kuisifia timu huku uhalisia ukiwavua nguo na kuwacha na boxer tu
 
Hv we mzee unadhani kufika robo fainali caf ni rahisi namna hiyo???aseee nyie watu sjui mnawazaga nini??
 
Mshaanza uganga???mtajuta kuwafahamu wasudan[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mpira na Mungu ni vitu mbilo tofauti labda mkatambike kwa majini tuu
 
Kama ulikua ujui Al hila wanasoma Albadiri saba kilasiku mpaka siku ya mechi,uchawi kwa wale ndo mwisho sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…