Wanaadamu wanaangamia kwa kukosa maarifa, Mpole anastahili kuwania uchezaji bora

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Bodi ya Ligi mnatusikitisha sana, mnatufanya tuwe na wasiwasi sana na uwezo wenu, yaani Bangala awanie mchezaji bora halafu F
George Mpole aachwe? Kwann mmetudharau sana watanzania kiasi hiki, mchezaji kutoka Geita Gold ya Mwanza, timu iliyopanda daraja msimu huu isiyo kuwa na wachezaji wa kimataifa, yenye kocha mswahili bado imetoa mfungaji bora msimu huu akiwa na mibao 17, amefunga kwenye mechi ngumu ikiwemo Simba ikiwa na mabeki wake wa kimataifa Inonga na Onyango, watanzania wote tumeona uwezo wa George Mpole, Leo mnatuambia hastahili kuwania tuzo ya mchezaji bora, jamani.
Bodi ya ligi wangeweza hata kusema mchezaji bora mwaka huu wagombanie akina Nyosso, Duchu na Abdi Banda bado tungekaa kimya maana hata hao waandishi hatuoni la maana wanalofanya, wao kila siku wanahoji bilioni 20 za Mo dewji.

Watanzania tuamke, serikali iingilie kati huu uhuni, George Mpole anastahili kuwania tuzo, yaani wacongo wote ndio wachezaji bora bongo, duh.Kweli tunangamia.
 
Geita haitok mwanza
 
Mayele ndiye mchezaji bora wa msimu ligi kuu msimu huu 2021/22 (My opinion)

[emoji419] Fiston Mayele ameipa ubingwa wa ngao ya jamii klabu yake ya Yanga kwa goli lake dhidi ya Simba SC.

[emoji419] Magoli (16) ya Fiston Mayele yamechangia points (35) kati ya points (74) zilizowapa ubingwa wa ligi kuu Young Africans.

[emoji419] Assists na Magoli yake yamechangia 37% ya ubingwa wa Yanga ligi kuu Tanzania bara.

[emoji419] Ndiye mshambuliaji pekee mwenye magoli mengi ambaye hajafunga goli la penati.

[emoji419] Mshambuliaji pekee kwenye tatu bora ambaye hana kadi yoyote ya njano.

[emoji419] Amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi mara mbili ligi kuu.

[emoji419] Moja ya Wachezaji waliotoa Assists nyingi
 
TFF wamefanya upuuzi mkubwa sana ktk hii selection ya uchezaji bora

Haiingii akilini George Mpole awe mfungaji bora wa ligi alafu asiwepo ktk kinyang'anyiro cha mchezaji bora,,, upuuzi mkubwa sana huu
 
Watanzania kazi mnayo dah,ktk siasa mnavurugwa.ktk mpira mnavurugwa pia
 
Hivi Yule Inonga Imekuwaje Anawania Uchezaji Bora Au Kwa Kumkaba Mayele Asifunge [emoji16]
 
yule mchezaji wa kawaida tu kiatu alichukua Son na kwenye premier na kwenye kikosi bora cha prenier hakuwepo itakuwa uyu sijui mpole[emoji4]
 
yule mchezaji wa kawaida tu kiatu alichukua Son na kwenye premier na kwenye kikosi bora cha prenier hakuwepo itakuwa uyu sijui mpole[emoji4]
Inawezekana watu hawafuatilii huko kwa wenzetu mambo yalivyoenda, alaf pia hizi tuzo wana vitu vingi vinaangaliwa sio magoli tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…