Wanabadilisha "Title Deeds"! mchongo mwingine?

Hebu mnisaidie wadau mie nilipotaka kuweka title deed ya shamba langu huko kisarawe nikaambiwa inabidi nichukue watu(afisa ardhi) waje wapime eneo kwanza kwa gharama zangu then ndo process iendelee,naomba kuuliza ni mie ninayetakiwa kuwasafirisha afisa ardhi na kuwalipia lunch ili wanipimie shamba au kuna fungu serikalini?wadau mliopima mashamba naomba mnisaidie
 
Balaa hizi pesa zinatakiwa ajili uchaguzi wa ccm hakuna lolote!!
 

Ni wizi wa wazi kabisaaaa hakuna ubishi!kuna mtu anafanya kamradi kake ili apate pesa za kampeni,Mwaka wa uchaguzi huu!
 
Wanatulazimisha kuwa masikini kwa nguvu zote, kama huna hela ya cheti kipya, inawezekana ukapoteza haki ya kumiliki sehemu, hivyo ukanyang'anywa hiyo sehemu akauziwa mtu mwingine!
 
Msiogope mabadiliko. Lazima twende na wakati. Tulianza na kusajili sim cards. Vitambulisho vya Lau navyo vyaja. Sasa tuna-ugrade Title Deeds. Ndio maendeleo hayo. Ya zama za Sayansi na Teknolojia.
 
Walipie na chenji/ vijisenti vya BAE...na vile vinavyoendelea kurudishwa walau kwa kudunduliza vya EPA.
 
180,000 za nini? Wanaweza ku break down matumizi yake?

Si waseme tu wanatafuta fedha ya uchaguzi kwa nguvu.
 

Mkuu bora wewe, mimi nilinunua kiwanja kule Kongowe-tuangoma ktk manispaa ya temeke mwaka 2005 kwenye ule mradi wa viwanja vya serikali.

Lakini nilipokuwa nafuatilia kibali cha ujenzi (building permit) nikaambiwa lazima nimpeleke afisa ardhi kwa gharama zangu akaangalie kama kweli kiwanja kiko salama sijajenga kitu hapo ndo waniandalie building permit.

Mimi niliwaambia kama mnataka pesa kwa mtindo huo kwangu hampati ng'o. Basi walinipigisha kwata kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka nipate kibali na hapo ni baada ya kumwambia mhandisi wa manispaa wakati ule (ndg. Mpapasingo) kwamba anachezea kazi yake.

Kwa ufupi serikali yote imeoza kwa rushwa na wizi.
 
Msiogope mabadiliko. Lazima twende na wakati. Tulianza na kusajili sim cards. Vitambulisho vya Lau navyo vyaja. Sasa tuna-ugrade Title Deeds. Ndio maendeleo hayo. Ya zama za Sayansi na Teknolojia.

Kilio cha watanzania wala siyo kuogopa gharama, mtanzania ni mtu mzuri sana kwa kulipia gharama tena zingine hajui hata analipia nini. Tatizo ni serikali kuwafanya wananchi kama wajinga kwamba wanalipia kitu kisicho julikana.
 
Msiogope mabadiliko. Lazima twende na wakati. Tulianza na kusajili sim cards. Vitambulisho vya Lau navyo vyaja. Sasa tuna-ugrade Title Deeds. Ndio maendeleo hayo. Ya zama za Sayansi na Teknolojia.

"For the choice is not between change or no change; the choice for Africa is between changing or being changed - changing our lives under our own direction, or being changed by the impact of forces outside our control" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere's Introduction to Freedom and Unity
 


Nakuaminia. Thanks. God bless and Protect you!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…