WanaCCM hawamuelewi Rais anasema kwenye maono gani, wao ni kupiga makofi tu

WanaCCM hawamuelewi Rais anasema kwenye maono gani, wao ni kupiga makofi tu

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Ilikuwa mnafanya siri na kuudanganya umma leo Mwenyezi Mungu amewaadhiri vibaya sana sana hamna pa kujificha.

Tena si kuudanganya umma wa Watanzania bali kuidanganya dunia nzima. Mnacheza na Mwenyezi Mungu atu dua zetu zimekubaliwa. Mmekwiba kura sawa tumepotezea, lakini kumsingizia Mwenyezi Mungu kwamba anawapenda CCM hilo litawapa tabu sana.

Tulikuwa tukijigamba kwamba nzige wameruka hawakutua Tanzania na hata corona tumeomba dua Mwenyezi mungu ameiondoa. Tatizo CCM wanajifanya too much know kumbe hawajui kitu without knowing.

CCM wanawaona waTz bado ni walewale wasioelewa. Sijui kwanini wanasahau kuwa sasa dunia ni kijiji kidogo sana.

Ndugu zanguni vaaeni barakoa na kama akitokea akawambia vueni, mtu huyo ni adui yenu na ondokeni hapo mwachieni jukwaa peke yake au ukumbi peke yake.

Sijawahi kumsikia Magufuli akiwaamrisha watu wavue barakoa. Najua anapingana nalo na vilevile analiunga mkono. Ukimfahamu ni kuwa tutengeneze mabarakoa hapahapa nchini na sio ya kutoka nje.

WanaCCM hawamuelewi Rais anasema kwenye maono gani, wao ni kumpigia makofi tu.
 
Back
Top Bottom