WanaCCM wana mengi kuhusu Hayati Magufuli, tutasikia mengi tuwe na akiba ya maneno

WanaCCM wana mengi kuhusu Hayati Magufuli, tutasikia mengi tuwe na akiba ya maneno

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari JF,

Ni wazi kuwa Rais Samia atashinda uchaguzi wa 2025 kwa namna yoyote ile. Hili liko wazi hata kwa wapinzani ambao tayari wamelielewa. Na hii sifia sifia ina ahadi nzuri ndani yake.

Hivyo, 2025 goli liko wazi kwa nafasi za ubunge na udiwani. Kitakachotokea ni kwamba wabunge wataingia bungeni kwa nguvu zao na madiwani pia haitajalisha chama iwe CCM au CHADEMA.

Kwa maana hiyo, hakutakuwa na unafiki na hapo ndipo tutasikia mengi sana kuhusu shujaa JPM yaliyokuwa yanaogopeka kusemwa.

Tuwe na akiba ya maneno, maana yajayo yanafurahisha. Lakini pia, 2025 goli liko wazi, vijana tuchangamkie fursa ya ajira ya siasa.
 
Back
Top Bottom