WanaCCM wengi tunataka serikali Tatu.

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
550
Tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani kuhusu mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya, kwa sasa wanaCCM wengi wenye uelewa mpana tunataka uwepo wa serikali ya Tatu ya Tanganyika.

Wakati kukiwa na juhudi na nguvu kubwa kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM 'kuwakaririsha' wanaCCM sehemu mbalimbali nchin ili waweze kwenda kusema mbele ya tume ya Katiba mpya kuwa wanataka serikali mbili, lakini hali inazidi kuwa mbaya na tofauti kwa wanaCCM wengi wenye uelewa ambao kwa dhati tunataka serikali Tatu.

Uchunguzi wangu binafsi nilioufanya toka semina za wanaCCM zianze ule wimbo wa kuwaimbisha wanaCCM kusema serikali mbili unaelekea kuchuja maana wengi wa wanaCCM wameshindwa kupata sababu za msingi kwanini iwe serikali mbili na wala sio serikali tatu kama rasimu ya katiba inavyopendekeza?
 
wengi wenye maamuzi ndani ya ccm hawa taki serekali tatu.....
viva tanganyika yetu.
 
wengi wenye maamuzi ndani ya ccm hawa taki serekali tatu.....
viva tanganyika yetu.

Nape yuko ITV anachapia..... eti CCM kama taasisi.ina maoni yao..... si walisha toa yakasikika.... sasa wana wasiwasi gani na vi-memo vya hapa na pale.... wawaache watu nao watoe yao kama watu binafsi.....!!!!
 
wengi wenye maamuzi ndani ya ccm hawa taki serekali tatu.....
viva tanganyika yetu.

Hayo umeyapata wapi? Kwa taarifa yako G55 ilikuwa na baraka zoote za Mwinyi. Wengi waliomo madarakani wameibuliwa na Mwinyi na Mkapa. Watafuata mawazo ya Wengi. Njelu Kasaka na Malechela ni miongoni mwao.
 
nimekuso mkuu....vipi nape anatumwa na nani?
 
sasa kama wanaCCm wengi mnataka serikali tatu kwa nini hamkusema kwenye kikao hadi chama kikapitisha serikali mbili wakati wengi wenu mko upande wa wananchi?
 
Nape yuko ITV anachapia..... eti CCM kama taasisi.ina maoni yao..... si walisha toa yakasikika.... sasa wana wasiwasi gani na vi-memo vya hapa na pale.... wawaache watu nao watoe yao kama watu binafsi.....!!!!

watanzania tulio wengi tuna itaka tanganyika...ila kuna sababu vipo nyuma ya pazia wakina Nape hawataki, na visingizio vyao kuwa ni garama.
 
Ccm wanajitia aibu. Ngoja mbabe akitangaza serikali tatu mwitikio utakuwa mkubwa kwa wananchi.
 
wengi wenye maamuzi ndani ya ccm hawa taki serekali tatu.....
viva tanganyika yetu.

Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa CCM hakuna demokrasia huwezi ukamlazimisha mtu afuate unachokitaka wewe hata kama ni mwanachama wa chama chako wakati naye amepewa haki ya kutoa maoni yake kama raia halafu wewe unamlazimisha afuate maoni yako.
 
tunataka ushahidi wa unayoyasema kwa takwimu siyo maneno ya kijiweni. uchunguzi umeufanya kwa njia ipi? kwa kusafiri? kwa kusikia mwenyewe? kwa kuambiwa? tupe data kamili
 
Sasa hiv na nyie hamtaki hii kitu.
Zidumu fikra za mwenyekiti wa chama.
 
Hayo umeyapata wapi? Kwa taarifa yako G55 ilikuwa na baraka zoote za Mwinyi. Wengi waliomo madarakani wameibuliwa na Mwinyi na Mkapa. Watafuata mawazo ya Wengi. Njelu Kasaka na Malechela ni miongoni mwao.
Kweli kabisa hao uliowataja ndio wanaojua machungu ya nchi hii na ninashukuru bado wako hai na wataiona Tanganyika yao waliyoipigania kwani Sinde Warioba hatawatupa.
Ni vigumu kuwaeleza watoto wa G55 ya akina Njelu Moses Mnauye (R,I,P) na Malecela W. J. Malecela kuwa kuwasemea Wanzanzibar kuwa tunawapenda ni picha iliyochuja na wana CCM wameshaishtukia na ni BOMU linalosubiri kuwalipukia mikononi kwani watashindwa wamtupie nani wakati kwani aliyelishupalia ni Katibu mwenezi
Hawa vijana nawakumbusha Filamu za kina BAD SPENCER.
TERRENCE HILL aliamua BOMU limlipukie baada ya kuona aliodhani ni MAADUI
zake awamalize KUMBE WOTE NI NDUGU (WaTanganyika) NA HAWAPASWI KUTUPIWA BOMU lililofyatuliwa safety pin Kilichufuata watafute hizo filamu

Last edited by a moderator:
Sioni jinsi gani serikali ya CCM itaingia kwenye bajeti ya mwaka 2014 kabla ya mchakato wa katiba ya tanganyika kuwa umeshaanza; Kwa kweli CCM haina jinsi bali kuridhia kurejeshwa rasmi Serikali ya Tanganyika, Serikali ambayo imekuwepo kwa njia ya kiini macho kwa miaka karibia 50; Karibu Tanganyika;
 
Watanganyika sasa mshakuwa hamumuogopi tena nyerere.
 
Muungano ni wa wananchi sio wa vyama. Hawa CCM wasitufanye Watanganyika mamburula. Wananchi wanataka serikali tatu ccm wawalisha wanachama wao maneno wakaongee kwenye mabaraza ya katiba bila aibu. Mwaka huu ni wa maumivu kwa mbele ndani ya CCM
 
Tanganyika inatakiwa na watangayika.CCM hawana hoja ya msingi kuzuia,ni blabla za kina Nape na wanaomtuma kwa maslahi yao na si ya Watanganyika.Ccm tuna freez na Tunairudisha TANU.bahati Kadi yangu ya Tanu sikuitupaga.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
wengi wenye maamuzi ndani ya ccm hawa taki serekali tatu.....<BR>viva tanganyika yetu.
Wakenya lazima watudharau sana hivi tunatengeneza katiba ya&nbsp;vyama au ya nchi miaka hamsini hadi mia ijayo!!mambo ya ccm kukataa serikali tatu yanatoka wapi???ccm kweli imefika mwisho hakuna hata mwenye ufahamu kuwa tunatengeneza katiba mpya ya nchi na sio ya chama fulani huo ni ubinafsi wa kudhani itatawala milele.
 
sasa kama wanaCCm wengi mnataka serikali tatu kwa nini hamkusema kwenye kikao hadi chama kikapitisha serikali mbili wakati wengi wenu mko upande wa wananchi?
Utaona wakati wa uchaguzi Safari hii hakuna kuchagua chama katika kupitisha katiba. Mfumo wa serikali tatu utashinda kwa kishindo. Kuwasikiliza viongozi wetu tunawasikiliza lakini twajua tutakavyochagua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…