WanaCCM wengi tunataka serikali Tatu.

Suala la serikali tatu haliepukiki, ni suala la muda tu.
 
Mleta uzi unajaribu kubackmail wasomaji, wewe sio mwana CCM hata kwa maneno yako tu.
Hapa serikali mbili tu.

1+1=2 :A S thumbs_up: :A S thumbs_up::amen:
If 1+1=3 you need:help:
 
Mleta uzi unajaribu kubackmail wasomaji, wewe sio mwana CCM hata kwa maneno yako tu.
Hapa serikali mbili tu.

1+1=2 :A S thumbs_up: :A S thumbs_up::amen:
If 1+1=3 you need:help:

Serikali Mbili ya Tanganyika na Either Ya Zanzibar ama ya Muungano.
 
Kwa kiasi kikubwa wale vinara wa kudai Serikali tatu wanasukumwa, hasa mambo makuu mawili:
1. Kwanza, ni Wazanzibari wenye msimamo mkali, na ambao wengi wao wanadhani wakipata Serikali ya Zanzibar yenye mamlaka kamili wataweza kupata manufaa kutoka nchi za kiarabu.
2. Pili, ni Watanganyika wakristo (wenye msimamo makali wenye udini)
na ambao wengi wao wanadhani kwa kutengana na Zanzibar watapata
nguvu zaidi ya kukamata nchi kwa ukamilifu na watanufaika zaidi
kama dini, hawa wanadhani hivi sasa Wazanzibar wanawaletea kiza.
 
tunataka ushahidi wa unayoyasema kwa takwimu siyo maneno ya kijiweni. uchunguzi umeufanya kwa njia ipi? kwa kusafiri? kwa kusikia mwenyewe? kwa kuambiwa? tupe data kamili

ww mpaka sasa unaweza kusema kwa kusiki mtaani jwenu,ofisini kwenu,darasani kwako,nyumbani kwako,n.k
kwangu mm,wengi ya niliowasikia hawataki serikali mbili!
 
watanzania tulio wengi tuna itaka tanganyika...ila kuna sababu vipo nyuma ya pazia wakina Nape hawataki, na visingizio vyao kuwa ni garama.
Kwani Nape anachangia kiasi gani katika hio gharama ? JK na wizi wenziwe au magamba wanachangia kiasi gani katika huu muungano ? Muungano unaishi kwa rasilimali watu wa Tanzania,na rasilimali za nchi ndani ya tanzania na misaada, mchango mkubwa unao tolewa na ccm /magamba au samaki, kuiba mali za umma, huo ndio mchango wao, kufa kwa ccm ni serikali tatu.,

Chadema unachukua Tanganyika, Zanzibar cuf, hapo na katika serikali ya muungano, tutapiga kura ndani ya bunge la muungano, tutaweka utaratibu maalum wa kupiga kura ndani ya kibunge cha muungano, badala ya kutumia rasilimali watu na rasilimali za nchi kumteuwa rais wa muungano, ni gharama ambazo tunaweza kupunguza.

Mambo matano kama tutayapunguza katika muungano tutaipunguzia mzigo mkubwa serikali ya muungano hata tanganyika na zanzibar zitapunguza gharama za kuchangia.

Uraia na uhamiaji
Benki na sarafu,
Vyama vya siasa.

Haya tunataka tuyaondoe katika orodha ya muungano, kwisha kabisa.
 

duchi ulichokiandika hapo sio sahihi kabisa.
Kwanza Zanzibar ni nchi kamili mpaka sasa, ziwe serikali mbili ama tatu bado Zanzibar inabaki kuwa nchi kamili. Wazanzibar wengi wanataka serikali tatu, na sababu kuu ni ili wawe huru zaidi. Mfumo wa serikali mbili unaminya uhuru wa Zanzibar.

Watanganyika wengi wanataka serikali tatu, na sababu inayowasukuma kudai hilo ambazo UHURU na UCHUMI. Why? Uwepo wa serikali tatu utarudisha uhuru wa Tanganyika uliokufa kutokana na muungano na itapunguza gharama za kuwatunza wazanzibar.
 
Last edited by a moderator:
We jamaa ngoja tukuandalie ban kwenye chama chetu.
Hufai kabisa yan unakiuka maagizo ya wakubwa?
 
Na iwe:

1.Serikali mbili= Tanganyika na Zanzibar

2. Serikali tatu=Tanganyika,Zanzibar na Muungano
 
wakuu serikali tatu ndo mpango mzima. mambo saba ya muungano yatapunguza sana gharama ya serikali ya muungano tofauti na magamba wanavyopotosha. tume ya warioba imefanya jambo jema sana kuyapunguuza na kuyarudisha kwa nchi washirika wa muungano.
 

well said mkuu...upo vizuri sana
 

tatizo la ccm wame weka uchama mbele kuliko utaifa [uzalendo]
 
Hii ni ishara ya kuonyesha kuwa CCM hakuna demokrasia huwezi ukamlazimisha mtu afuate unachokitaka wewe hata kama ni mwanachama wa chama chako wakati naye amepewa haki ya kutoa maoni yake kama raia halafu wewe unamlazimisha afuate maoni yako.

mkuu tatizo ni uroho wa madaraka..ccm wanafanya kama katiba ni yao.
 
Hello Chuki cjui umri wako ningekusaidia lakini serikali 2 ndo zimeshndwa,bado akili inakuwazisha hizo tu,bado ukoanalog
 
Muungano siyo hisabati wala ndoa bali makubaliano baina ya pande mbili yaani Zanzibar na Tanganyika.Hawa waliokaririshwa 1+1=2 uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo. Muungano wa mataifa mawili yenye historia tofauti, utamaduni,ukubwa wa eneo,uchumi,aina ya watu na mfumo wa siasa zake hatuangalii mahesabu kwani hayana ukweli wenye kudumisha muungano nje ya kuongeza kero. Mfano, ukubwa wa eneo la Zanzibar na Imani za watu wake wengi si sawa na Tanganyika hivyo haiwezekani Zanzibar ikabeba 1 na Tanganyika ikawa na 1 vilevile. Usawa wa Tanganyika na Zanzibar ungekuwepo kama tungekuwa sawa na hapo 1+1= 2 ingekuwa relevant. Huwezi kuchukua Mbuzi 1+1 Ng'ombe = 2 kwa kuwa tu eti yote ni mifugo yenye historia sawa ya kufugwa na binadamu na kulishwa nyasi.Ni lazima utafute utaratibu mwingine ili ufuge vema.Hapa serikali 3 ni jawabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…