Wanachama wa TALGWU mwaka huu tunapigwa, no tisheti wala kofia

Wanachama wa TALGWU mwaka huu tunapigwa, no tisheti wala kofia

Mastamind

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,304
Reaction score
830
Kuna Dalili ya Kuingia Sherehe za May Mosi Bila Kuwa na Jezi za TALGWU.

Mpaka leo April 29 hakuna mzigo wa kofia wala tisheti ulioingia na kugawiwa, viongoz dako kimya. Inaonekana Wako Kuvutana Aina ya Tsheti. Kweli Mwaka Mzima Hamjaamua ni zipi zakununua, Me naona kuna kajambo wanataka kukafanya watupge hata hz za jezi

Naomba anayejua vile namna yakujitoa kwenye hili chama lao maana toka niingie sijawahi ona faida yake, matatizo lukuki ya wafanyakazi, kunyanyaswa, kubambikiwa case, likizo na kuhamishwa bila malipo lakin hakuna wanachotetea.

Message ya Saa Hii:
watumishi na wanachama wa TALGWU mkoa wa Morogoro. Tarehe 29/4/2022.
YAH. SARE (T-SHIRT) ZA MEIMOSI MWAKA 2022.
Kila mwaka watumishi kote duniani huadhomisha sherehe za meimosi. Madhimisho haya kwa kawaida huenda sambamba na ugawaji wa sare (t-shirt) za meimosi kwa wanachama wa kila chama Cha wafanyakazi. Kwa msingi huo baai:-
1. Naaikitika kuwataarifu wanachama wa TALGWU mkoa wa Morogoro kwamba siku ya meimosi kwa maana ya tarehe 1/5/2022 hatutakuwa na sare za meimosi za mwaka 2022. Hii ni kwa sababu tisheti zilizotengenezwa na kusambazwa mikoa yote ya Tanzania bara haziko kwenye ubora unaotakiwa ambao sisi viongozi tulipendekeza na tukakubaliana. Kwa mantiki hiyo sisi wenyeviti mikoa yote tukawa na msimamo kuzikataa hizo tisheti kutokana nabubovu wake na hazitagawiwa kwa mwanacha yeyote na zimerudishwa hq kwa ajiri ya kuridishwa kwa mzabuni.
2. Hatua zimechukuliwa za haraka kutengeneza sare (t-shirt) zingine ambazo zenye ubora tunao uhitaji na zitaanza kusambazwa kesho kwa kuanza na wilaya ambako meimosi inaazimishwa kimkoa. Kwa mkoa wa Morogoro meimosi kimkoa inaazimishwa wilaya ya Kilosa mji mdogo wa mikumi. Hata hivyo kutokana baada ya meimosi sare zitaindelea kutengenezwa na baadae kusambazwa kwa mikoani na baadae kwa wanachama wetu ingawa hatutazivaa siku ya maazimisho.
3. Kwa niaba ya chama Cha Talgwu mkoa wa Morogoro. Nitumie fulsa hii kuwaomba radhi watumishi na wanachama wote mkoa wa Morogoro. Changamoto hutokea mara popote lakini pia ndo husaidia kufanya maboresho. Kwa hiyo ninaomba muwe watulivu swala la sare linashugulikiwa kwa haraka.
5. Pamoja na changamoto hii sisi viongozi wenu imetuumiza mno. Niwaombe kwa heshima zote. Siku ya meimosi tunaweza kuvaa sare zetu za mwaka Jana kwa aliye nayo sare yoyote anaweza kuvaa.
Mwisho nawatakieni maandalizi na maazimisho mema ya sikukuu ya wafanyakazi Duniani kote. Mungu akasimame na mama aweze kutoa tamko lenye neema.

Wanazidi Kunikasirisha tu[emoji35]
 
Andika barua kwa akutoe, au ongea na kumpanga Hr yoyote anayeweza ku access mfumo akutoe, kwanza ukifuatilia Ma Hr wengi awapo kwenye iyo TALGU, ni wajinga wajinga hawana msaada
 
hata sisi tunaofanya vyuo vikuu chama chetu cha THTU wametoa mafulana mabaya kweli
 
Vyama vingi vya wafanyakazi ni tatizo kwenye nchi yetu. Badala ya kupigania maslahi na haki za wafanyakazi vyenyewe vimejikita kwenye kugawa kofia, fulana na vitenge wakati wa sherehe za kitaifa. Wakati mwingine hata kutoa msaada wa kisheria kwa wafanyakazi pale wanapohitaji hawasaidiwi japo ni takwa la lazima kutokana na mfanyakazi kutoa michango yake kila mwezi. Lakini wa kulaumiwa hapa ni wafanyakazi wenyewe kwani wao ndio wanawaweka madarakani hao viongozi. Na hata ikitokea kukawa na viongozi imara bado wafanyakzai hawawalindi wala kuwapigania pale wanapotaka kuondolewa kwa hila. Kila nikifiria kilichotokea kwenye chama cha walimu miaka michache iliyopita nashindwa kuelewa. Chama cha walimu kilikuwa imara sana wakati wa uongozi wa Gratian Mukoba na Oluoch sijui kilitokea nini kwani sasa kimebaki tu jina tu.

Mimi binafsi kwa upande wangu nilijitoa kwenye chama cha wafanyakazi baada ya kuona vipaumbele vya viongozi ni kugawa tshirt, kofia na vitenge. Kila ikitokea kesi kati ya mwajiri na mfanyakazi viongozi wanaegemea upande wa mwajiri badala ya kusimama katii kati ili haki ijulikane ipo kwa nani. Hapo ndio nilipoona huu ni ujinga nikasema ile pesa ya mchango wa kila mwezi bora hata hata nikanunuae luku au kulipia bili ya maji kila mwezi. Na ikitokea kuna tatizo nitaingia mfukoni mwangu kutafuta msaada wa kisheria na kama sitakuwa na pesa basi nitaenda kwenye yale mashirika yanayotoa msaada wa kisheria bure.
 
Mwaka huu hata TUGHE ofisini kwetu imewapiga na kitu kizito wanachama wake sema bosi wetu kaokoa jahazi katoa pesa za ofisini kigharamia sherehe.
Mimi binafsi hakuna chama kinaweza kunishawishi nijiunge nao.
 
Kuna Dalili ya Kuingia Sherehe za May Mosi Bila Kuwa na Jezi za TALGWU.

Mpaka leo April 29 hakuna mzigo wa kofia wala tisheti ulioingia na kugawiwa, viongoz dako kimya. Inaonekana Wako Kuvutana Aina ya Tsheti. Kweli Mwaka Mzima Hamjaamua ni zipi zakununua, Me naona kuna kajambo wanataka kukafanya watupge hata hz za jezi

Naomba anayejua vile namna yakujitoa kwenye hili chama lao maana toka niingie sijawahi ona faida yake, matatizo lukuki ya wafanyakazi, kunyanyaswa, kubambikiwa case, likizo na kuhamishwa bila malipo lakin hakuna wanachotetea.
Kwani hua mnapewa bure? Mbona huwa mnakatwa kwenye mishahara wwnu?.
 
Vyama vingi vya wafanyakazi ni tatizo kwenye nchi yetu. Badala ya kupigania maslahi na haki za wafanyakazi vyenyewe vimejikita kwenye kugawa kofia, fulana na vitenge wakati wa sherehe za kitaifa. Wakati mwingine hata kutoa msaada wa kisheria kwa wafanyakazi pale wanapohitaji hawasaidiwi japo ni takwa la lazima kutokana na mfanyakazi kutoa michango yake kila mwezi. Lakini wa kulaumiwa hapa ni wafanyakazi wenyewe kwani wao ndio wanawaweka madarakani hao viongozi. Na hata ikitokea kukawa na viongozi imara bado wafanyakzai hawawalindi wala kuwapigania pale wanapotaka kuondolewa kwa hila. Kila nikifiria kilichotokea kwenye chama cha walimu miaka michache iliyopita nashindwa kuelewa. Chama cha walimu kilikuwa imara sana wakati wa uongozi wa Gratian Mukoba na Oluoch sijui kilitokea nini kwani sasa kimebaki tu jina tu.

Mimi binafsi kwa upande wangu nilijitoa kwenye chama cha wafanyakazi baada ya kuona vipaumbele vya viongozi ni kugawa tshirt, kofia na vitenge. Kila ikitokea kesi kati ya mwajiri na mfanyakazi viongozi wanaegemea upande wa mwajiri badala ya kusimama katii kati ili haki ijulikane ipo kwa nani. Hapo ndio nilipoona huu ni ujinga nikasema ile pesa ya mchango wa kila mwezi bora hata hata nikanunuae luku au kulipia bili ya maji kila mwezi. Na ikitokea kuna tatizo nitaingia mfukoni mwangu kutafuta msaada wa kisheria na kama sitakuwa na pesa basi nitaenda kwenye yale mashirika yanayotoa msaada wa kisheria bure.
Ulijitoaje mkuu?
 
Mimi binafsi nilishagoma washanifata viongozi mpaka wamechoka ukiangalia havina tija ivyo vyama wafanyakazi wanapata matatizo lakini hawatoi msaada wowote kazi kuangalia matumbo yao sina mpango wa kujiunga na chama cha wafanyakazi chochote
 
Tanzania Local Government Workers Union (TALGWU)

Kumbe hizo fulana huwa ni muhimu hivi,, kuliko maslahi yenu...

Wafanyakazi wa hii nchi ni nani aliyewaroga...
 
Tanzania Local Government Workers Union (TALGWU)

Kumbe hizo fulana huwa ni muhimu hivi,, kuliko maslahi yenu...

Wafanyakazi wa hii nchi ni nani aliyewaroga...
Umewaza Kama mimi mkuu. Binafsi nilidhani kwa kipindi hiki wangewekeza nguvu kubwa kudai maslahi yao na kupigania haki zao za msingi Kama annual incriment kupandishwa madaraja kwa wakati nk. T-shirt Ni nonsense kabisa.

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom